WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya
Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya
uhaba wa madawati na viti na kusababisha baadhi yao kuwa tabia ya utoro
kwa sasa wameanza kunufaika na agizo la Rais Dr.John Magufuli la kutaka
wanafunzi wote nchini kuhakikisha wanasoma wakiwa wamekaa kwenye
madawati.
Agizo hilo la Rais limetekelezwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini
Hamoud Jumaa kupitia kupitia fedha ambazo zimepatikana kutokana na
kubana matumizi yasiyo ya lazima katika ofisi yake kwa lengo la kuweza
kusaidia katika kuboresha sekta ya elimu.
Akikabidhi jumla ya madawati 537 Mbunge wa Jimbo hilo kwa uongozi wa
halmashauri ya kibaha vijijini katika halfa fupi zilizofanyika katika
shule ya sekondari kilangalanga iliyopo Mlandizi, amesema kwamba ametoa
madawati hao pamoja na vitabu kwa lengo la kuweza kupunguza kero na
kuondokana na adha ambayo walikuwa wanaipata wanafunzi wa jimbo lake
katika siku za nyuma.
Kwa upande wake Afisa elimu katika halmashauri ya kibaha vijijini Coskansia Mafuru amebainisha kwamba awali kabla ya agizo la Rais walikuwa wana upungufu wa madawati 1923 kwa shule za msingi, hivyo msaada huo utaweza kumaliza changamoto zilizokuwa zikiwakabili na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Post a Comment