0

 
Kuna baadhi ya watu mbalimbali waliweza kueleza maana ya umaskini kutokana na wao wanavyoelewa. Wapo baadhi ya watu walisema kuwa umaskini hutokana mtu kuishi chini ya dola moja kwa siku. Wapo pia waliosema kuwa  neno umaskini halina maana sahihi kutokana na kila msomi alivyokuwa na tafsiri yake.

Tuachane na hayo na kuacha kila mmoja aweze kubaki na maana ambayo kila mmoja aweze kuelewa  mwenyewe kutoka  na anavyoona jinsi maisha yake na jamii kwa ujumla. Fuatana nami katika muda huu ili uweze kujua mbinu za kukutoa kwenye umaskini hadi utajiri.

Zifuatazo ndizo mbinu za kukutoa kwenye umaskini hadi utajiri.

1. Kuondokana na dhana  potofu.
Moja ya changamoto ambayo inatukumbuka wengi ni kuishi katika kuamini ya kwamba ni lazima ujihusishe na masuala ya kishirikina ili ufanikiwe zaidi. Misingi hiyo endapo utaishi nayo na kukua nayo itakufanya uamini ya kuwa maisha ya mafanikio hayapatikani kwa njia njia nyingne isipokuwa ushirikina. Ila ukweli ni kwamba mafanikio ya kweli yanapatikana kwa wewe kufanya kazi kwa bidii.

Kila jambo linahitaji juhudi za kiutendaji na si vinginevyo. Mafanikio yanayopatikana kwa njia ya ushirikina ni njia ya mkato yenye madhara makubwa ndani ya muda mfupi kama unabisha jaribu kufanya hivyo uone. Ukitaka kufanikiwa zaidi jambo la msingi ni  kufikiri mara mbili na kwa umakini wa hali ya juu huku ukibadili mtazamo .


Ondokana na dhana potofu zinazokuzuia kupata pesa.

2. Kujiamini kwa jambo lolote.
Kwa kuwa wewe ndiye msaka tonge kwa kutumia mbinu halali  za kimafanikio huku ukiongeza juhudi na ubunifu katika utendaji wako wa kazi huku ukiamini ya kwamba wewe ni zaidi ya watu mabilionea. Unajua kwa nini nimesema hivyo? ni kwa sababu wengi wetu hatuamini katika kazi ambazo tunazifanya.

Ukichunguza kwa umakini tofauti kubwa kati ya maskini na tajiri utagundua katika kauli zao.  Maskini akiwa anaenda kufanya kazi zake utashangaa wakati anaaga utamsikia naenda kuhangaika. Au ukimpigia simu ukimuuliza upo wapi kwa sasa utamsikia nipo kwenye mihangaiko tu ndugu yangu. Wakati kwa upande wa tajiri huwa ni kinyume chake ukimuuliza upo wapi atakwambia nipo kazini. Na asubuhi utamsikia naenda ofisi.

Ukichunguza kwa umakini katika kauli hizo utagundua ya kwamba maskini ni mtu wa kutojiamini hata kidogo wakati wewe una uwezo wa kutengeneza kipato zaidi ya huyo anayesema naenda kazini. Ewe Msomaji wa makala haya endapo utaendelea na kauli zako hizo ya kwamba naenda kwenye mihangaiko ni kweli utahangaika mpaka pumzi itapokata hivyo ni wakati wako sahihi wa kubadili kauli zako kwa kusema huku unajiamini, na wewe unaenda kazini na ofisini.

3. Kubali kukosolewa
Huwa nafurahi sana hasa pale tunapokutana na marafiki zangu tukiwa tunazungumzia mchezo wa mpira wa miguu. Huwa tunakuwa na hoja mbalimbali na kusema fulani kabebwa, huku wengine wakisema yaani leo kocha angemchezesha fulani ingewezekana tungeshinda. Unajua ni kwa nini nimekupa kisa hicho ukweli ni kwamba watu wanakuzunguka ni wazuri sana katika kugundua jambo ambalo unalolifanya   kwa kuona mapungufu na mazuri iliyonayo. Hivyo ni muda wako sahihi wa kuchukua maoni yao na kuweza kuyafanyia kazi ili kuweza kuboresha ofisi au jambo lako.

Ewe msaka Mafanikio kumbuka ya kwamba tumia kidogo ulicho nacho ili kupata mafanikio zaidi.

Post a Comment

 
Top