Mkuu wa Kamati ya
Kimataifa ya Olimpiki,Thomas Bach,ametangaza kwamba udanganyifu wa
utumizi wa dawa za kulevya katika michuano ya Rio tabia hiyo itakuwa
haina mahali pa kujificha.
Akizungumza katika usiku wa kuelekea
katika sherehe za ufunguzi,Mr Bach amesema kwamba wakati wa michuano
hiyo maelfu ya vipimo vitafanywa ,na sampuli za vipimo hivyo
zitahifadhiwa kwa miaka kumi ijayo , na kusema kwamba atahakikisha
watumizi wote wa dawa za kusisimua misuli kamwe hawatakuwa salama.Bach Aliongeza kusema kuwa takwimu ya mwisho juu ya idadi ya wanariadha wa Urusi ambao wataruhusiwa kushiriki katika michuano hiyo ya michezo ya Olimpiki watatangazwa saa chache zijazo.
Wakala wa kuzuiautumizi wa dawa za kusisimua misuli imependekeza kuwa yeyote atakayekutwa ametumia dawa hizo wapigwe marufuku katika michuano hiyo chini ya mpango wa ufadhili wa serikali ,ingawa Kamati ya Olimpiki ya Urusi imesema kwamba wanamichezo wake wapatao mia mbili na sabini na mmoja wamesha thibitishwa kushiriki katika michuano hiyo ya Olimpiki
Post a Comment