Wananchi,viongozi wa serikali ya kijiji
wakifukua kaburi la mtoto mwenye ualbino katika kijiji cha Bunambiyu
wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga
Askari polisi akishiriki zoezi la kufukua kaburi la mtoto huyo
***
Habari kutoka Kishapu mkoani Shinyanga
zinaarifu kuwa kaburi alilozikwa mtoto mwenye albinism Michael Juma
mwenye umri wa miaka miwili na nusu, mkazi wa kijiji cha Bunambiyu
kata ya Bunambiyu wilaya ya Kishapu aliyefariki dunia siku ya Jumamosi
wiki iliyopita, limefukuliwa kisha kuzikwa tena.
Hatua ya mwili huo kufukuliwa imekuja
baada ya kuibuka utata uliohusisha imani za kishirikina kwamba baadhi ya
viungo vya mwili wa mtoto huo havipo.
Mwili wa mtoto huyo kwa mara ya kwanza ulizikwa siku ya Jumapili wiki
iliyopita kisha kufukuliwa na kuzikwa upya siku ya Alhamis Agosti 18
mwaka huu baada ya Mahakama kutoa kibali mwili ufukuliwe ili kumaliza
utata ulioibuka.
Akizungumza kabla ya kufukua mwili huo, katibu wa chama cha watu
wenye ualbino mkoa wa Shinyanga Lazaro Anael amesema marehemu
alizikwa akiwa na viungo vyake vyote vya mwili na wazazi ,viongozi wa
kijiji na kata walijiridhisha kwa kuuona mwili na hakuna kiungo
kilichokatwa.
Amesema cha kushangaza baada ya mazishi alipigiwa simu na mkurugenzi wa
shirika la Under The Same Sun Vick Ntetema aliyekuwepo hata siku ya
mazishi akimueleza kuwa kaburi la mtoto huyo linatakiwa kufukuliwa kwa
madai kuwa kuna utata umejitokeza.
Mzazi wa marehemu Juma Masudi amesema mwanae alifariki Siku ya
Jumamosi Agosti 13,2016 na kuzikwa Agosti 14 mwaka huu baada ya kuugua
na hakuna kiungo cha mtoto kilichokatwa.
Baada ya kufukua kaburi hilo daktari Helena Kaunda kutoka kituo cha afya
Bunambiyu alisema viungo vyote vya mwili viko sawa na hakuna
kilichokatwa hivyo mwili wa marehemu ukazikwa tena.malunde blog
Post a Comment