0

Pengine umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Yako mambo mengi ya kufanya mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.Viko vitabu vingi na tena siku hizi zinatolewa DVD za jinsi ya kufanikiwa katika maisha. Utashangaa mpaka unamaliza kusoma au kutazama DVD hizo hujapata njia ya wazi sana sana utajilaumu tu kwa kuendelea kupoteza fedha kwa kuchangia miradi ya wajanja hao.

Wengine wanakuambia "amini tu kuwa wewe ni tajiri na utafanikiwa" mh! INAWEZEKANA? Afadhali hao, balaa zaidi ni wale ambao wanayanadi mafanikikio na utajiri kwa mizizi, hirizi na hata roho za binadamu wenzao!

Somo langu ni dogo lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana. Sasas kuwa makini zaidi. Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo. Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4 . Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa makoo(majike) watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga. Utakuwa na kuku 200 + 25 =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700. Ndugu mwanajamvi hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000. Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku 1,000. Mwaka 2. 750(majike) x 10 = 7500 (uza wengine) 3000 x 10 = 30,000. Kutegemea na uwezo wako mpaka mwisho wa mwaka wa pili utakuwa umefanikiwa sana. Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi huku ukiacha kando uzushi wa vitabu vya wasanii na DVD zao pia. NB. Kumbuka kuku ninao wazungumzia hapa ni wale wa kawaida sio wale mataahira (wa kisasa).Fuatilia zaidi kuhusu matibabu na matunzo mengineyo..

Post a Comment

 
Top