0

Viumbe hawa wanasifa nyingi zinazofanana kwa ukaribu sana kama utaamua kuwachunguza kwa ukaribu utagundua mambo mengi kuhusu hawa jamaa, ingawa pia zipo mbinu nyingi na namna mbalimbali za kujenga au kuanzisha uhusiano.

1: Viumbe hawa wa aina mbili wana sifa kadhaa za awali zinazofanana na moja ya sifa yao ni kwamba wote upatikana katika mazingira yetu ya kawaida yawezakuwa ni sehemu zetu za kazi,mtaani kwako, shuleni/Vyuoni au katikati ya safari(ndani ya bus) au kwenye tukio fulani pia hata kwenye mitandao ya kijamii ambapo ukaribu baina ya mtu na mtu yamefanywa kuwa rahisi sana katika karne hii, kimsingi zipo njia nyingi sana za awali katika kujenga mauhusiano kati ya mtu na mtu kwa ufupi ni kwamba hawa jamaa wanapatikana kila kona ya maisha yako na wote ni  walimu wazuri katika kuyajenga maisha yako.

2: Wote ni wacheshi, wachangamfu, watani kiasi chake, wanaupendo na mambo mengine kadha wa kadha ingawa sifa zote hizi zina viwango tofauti kulingana na ukaribu wako na watu hawa.
Najua unaweza kuwa na watu wengi sana unaowaita marafiki, watu ambao umekuwa nao kwa kitambo kidogo au kwa kipindi kirefu yamkini wapo ambao umekuwa nao tangu utoto wako na mpaka leo bado mpo pamoja na wengine umekutana nao katikati ya safari kuelekea huko uendako na kuwakaribisha au kukaribishwa wawe pamoja nawe na kujiaminisha kwa dhati kabisa uwezi kufika na kutimiza haja ya nafsi yako pasipo uwepo wao .

Ipo hivi siyo wote uliona nao ni marafiki wa kweli namaanisha kuwa umechanganya mchele na pumba pasipo kujua hama unajua lakini naomba ujue kuwa siyo dhambi kuchanganya kwani hapo juu nimekueleza kuwa wote wanasababu sababishi ya kuyaakisi maisha yako kwa kukuletea FURAHA hama HUZUNI ila usipende kusema kuwa wamekuleta huzuni tafadhali penda kusema  kuwa wamekupa FUNDISHO kwani napenda ujue kuwa uwezi kujifunza pasipo watu kuyazunguka maisha yako sasa yapo mambo mengi sana katika huu mzunguko, Narudia tena, "uwezi kujifunza pasipo watu kuyazunguka maisha yako by Hilary Geofrey Mbonde teh tehe".

Sasa utajuaje kuwa huyu ni rafiki au kampani, ipo hivi:-

1. Kampani hana sifa ya kuishi na wewe kwa muda mrefu.
Huyu jamaa uja na kuondoka ni kama nyimbo za Bongo Flavour au kama alivyokuja CHURA kisha akapotea, dah jamani Chura teh teh teh. Naomba ufahamu kuwa huyu jamaa uja kwako kwa sababu maalum na kisha ataondoka na kukuacha baada ya utimilisho wa sababu zake, nafikiri zaidi ya 90% ya hawa jamaa daima uwamba ngoma kuvutia kwao kama unabisha waulize wazee wa VITI virefu au waulize wazee wa timu POPO wao wana takwimu nzuri zaidi. Kama utaki kuwauliza wazee wa viti virefu au timu popo basi jiulize mwenye wangapi ulikuwa nao katika ufalme wako lakini leo hii haupo nao tena,sikia ipo hivi rafiki akuachi. Friend in need is the friend indeed.

2. Kampani ana sifa hii katika mawasiliano, 
Tafiti zinaonyesha kuwa hisia za urafiki ukua na kuimarika au ubomoka kutokana jinsi watu wanavyowasiliana mara kwa mara. Sasa ukiona mawasiliano yako siyo mazuri au yanayumbayumba wewe na rafiki yako basi ujue huyo ni KAMPANI tu na siyo rafiki wa kweli. kuna mifano mingi sana unaweza kuitumia katika kuelezea falsaha hii lakini ebu yumia mfano huu kuangalia mahusiano ya kimapenzi, nini kinatokea baada ya muda fulani pale rafiki X anaposhirikiana katika kuukimbiza mwenge na rafiki Y. Ukiona mawasiliano yanayumba baada ya mbio za mwenge kuisha ujue kuwa huyo rafiki X  au rafiki Y alikuwa ni KAMPANI tu.

3. Kampani ana sifa hii katika mazingira ya shule/vyuoni/kazini na sehemu nyingine zifananazo na hizi,
Mara nyingi huwa wanaogopa/kuhofia kujitegemea au kujisimamia ndiyo maana wamekuwa watu wa kutafuta mtu/watu wa karibu ili wawasaidiane katika masomo kwa kuwa ni magumu(wao uamini hivyo) au kazi fulani na mahusiano haya ya kusaidiana uweza kudumu kwa muda mrefu sana mpaka ukahisi YES huyu niliyempata ni rafiki wa kweli. Ebu jiulize ni watu wa wangapi uliowai kuwaita marafiki katika mazingira yako ya shule au kazini n.k lakini leo hii haupo nao tena, teh teh hao walikuwa ni KAMPANIi tu kwani marafiki wa kweli narudia tena marafiki wa kweli huwa awaachani, daima ukumbukana na uendelea kusaidiana katika mazingira yoyote. Ipo hivi, Eagles fly with Eagles.

Sikia sisemi uachane nao kwa maana maneno yangu siyo sheria lakini ukiona vema unaweza ukayazingatia. Sasa Rafiki wa kweli ni kinyume cha hizo sifa kuu tatuhapo juu lakini pia auhitaji kutumia akili au nguvu nyingi sana kuwajua/kumjua kwani swahili wanasema "Mapenzi ni kikohozi", jambo lolote kabla ya kutokea uanzia na fikra basi rafiki wa kweli ni mjenzi wa fikra chanya. Ipo hivi, rafiki wa kweli ana sifa fulani uliyokaribiana na upendo wa mama, nimesema iliyokaribiana.

Post a Comment

 
Top