0

Utawala nchini Uturuki unasema umefunga zaidi ya mashirika 2000 yenye uhusiano na kiongozi wa dini anayeishi nchini Marekani Fethullah Gulen, ambaye analaumiwa kwa kupanga mapinduzi ya kijeshi yaliyozimwa wiki iliyopita.
Amekana kuhusika . Kati ya mashirika yaliyofungwa ni pamoja na vituo vya afya na zaidi ya shule 1000 za kibinafsi.
Hatua hizo zimechukuliwa kama moja ya jitihada kubwa za kukabiliana na mitandao inayomuunga mkono bwana Gulen.
Maelfu ya wanajeshi, polisi na watu wengine wamekamatwa.

Post a Comment

 
Top