July 16 2016 ilikuwa ni zamu ya wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa klabu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wao wa tatu wa Kundi A wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya klabu ya Medeama SC ya Ghana.
Kabla hata ya mchezo wa leo July 16 Yanga walikuwa nafasi ya mwisho kutokana na kukubali vipigo viwili mfululizo vya michezo yao miwili ya mwanzo, mchezo wa kwanza Yanga walicheza Algeria na MO Bejaia na kukubali kipigo cha goli 1-0 na baadae kipigo cha goli 1-0 kutoka TP Mazembe ya Congo uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Mchezo wa July 16 Yanga wanaofundishwa na kocha wao muholanzi Hans van der Pluijm,
walikuwa wanahitaji ushindi wa aina yoyote ili waweze kuwa katika
nafasi nzuri zaidi ya kuwania kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano
hiyo, hata hivyo Yanga wamelazimishwa sare ya goli 1-1.
Kikosi cha Yanga
ambacho kilionekana kuwa na morali ya kuondoka na point tatu na
kusahaulisha mashabiki wake vipigo viwili vya mwanzo, walianza kupata
goli dakika ya 2 kupitia kwa Donald Ngoma ambaye alitumia vyema pasi ya mzimbabwe mwenzake Thabani Kamusoko, furaha ya Yanga ilizimwa dakika ya 17 baada ya Benard Danso kuisawazishia Medeama goli na kuifanya Yanga endelea kuwa nafasi ya mwisho katika msimamo wa Kundi A.
Post a Comment