0


Hali ya wasiwasi imetanda kwenye vijiji vya tarafa ya Loliondo baada ya watu kumi na sita wakiwemo wenyeviti wawili wa vijiji vya Mondoros na Keitaro pamoja afisa sheria mfawidhi wa kituo cha sheria na haki za binadamu mkoa wa Arusha Shilinde Ngalula kudaiwa kukamatwa kwa madai ya kujihusisha na matendo ya ujasusi huku wananchi wakidai kuwa kinacho wafanya kukamatwa ni kukataa kutoa ardhi yao kwa wawekzaji kutoka nje ya nchi.

ITV ilifika kwenye vijiji vya Ketaro Oloipiri Ololosokwani Ololieni lopol Oldonyowasi Losoito Arusha na kushuhudia ukimya uliyo tawala kwenye vijiji hivyo huku wananchi wakiogopa kuongea hata na waandishi wa habari kwa hofu ya kukamatwa.

Kwa upande wake afisa sheria mfawidhi na mkuu wa kituo wa kituo cha sheria na haki za binadamu mkoa wa Arusha Shilinde Ngalula amesema alikuja Loliondo kutetea watu waliyo kamatwa na kuelezea alichokutana nacho.

ITV iliutafuta uongozi wa juu wa mkoa wa Arusha na kubisha hodi kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Ntibenda kupata ufafanuzi wa matukio hayo lakini wasaidizi wake wamesema yupo mkoani Dodoma kwa shughuli za kiofisi lakini juhudi zaidi za kumpata kiongozi huyo zinaendelea.

Post a Comment

 
Top