0
PombeWataalamu wanasema hakuna kiwango salama cha unywaji pombe
Utafiti mpya imedokeza kwamba kuna uhusiano mkubwa baina ya unywaji pombe na aina saba za saratani.
Matokeo ya utafiti huo yaliyochapishwa katika jarida la "Addiction" yanaonyesha kuna uhusiano mkubwa wa moja kwa moja kati ya unywaji pombe na madhara ya kiafya ingawa bado haijabainika hilo linatokea vipi kibiolojia.
Saratani ambazo imegunduliwa zina uhusiano mkubwa na unywaji pombe ni pamoja na saratani ya mdomo na koo, saratani ya kikoromeo, saratani ya ini, saratani ya utumbo mpana, saratani ya matumbo na saratani ya matiti.
Mwezi Januari mwaka huu, afisa mkuu wa matibabu nchini Uingereza alitahadharisha kwamba hakuna kiwango chochote cha unywaji pombe ambacho hakina madhara kwa mwili.
Unywaji pombe unakadiriwa kusababisha vifo vya watu 500,000 kutokana na saratani mwaka 2012 pekee.

Post a Comment

 
Top