Zaidi ya nusu saa nilikuwa tayari
nimepoteza mule ndani ni kitafakari mazungumzo yale ambayo kwa kiasi kikubwa
mjomba alikuwa akilalama kuhusu tabia mbovu aliyoanzisha mkewe mwishowe
kumkimbia kabisa huku akimuachia mtoto.
Mara nilianza kusikia sauti ya mama
ikiniita, haraka nilijitoa mule ndani huku nikijiweka kwenye mtazamo mwingine,
mtazamo ambao ingekuwa ngumu mama kujua hali yangu. Ilinibidi nijiweke vile,
nilishamzoea mama yangu mara nyingi huwa ni mwepesi kubaini hali yangu, hivyo
ingenisababishia maswali mengi ambayo kwa muda ule ningekosa majibu ya kumjibu.
Baada ya kujihakikisha niko sawa nilijitoa ndani kana kwamba hakuna kilichokuwa
kinanitatiza.
Ukweli nilifanikiwa kumhadaa mama
kabla ya kuniambia nimsindikize mjomba, jambo ambalo nilikuwa nalihitaji sana
maana ndio ingeweza kunipatia walau majibu ya kile kilichokuwemo kwenye kichwa
changu.
Wakati huo, jua lilikuwa limebakisha
masaa kadhaa kabla utawala wa giza kuingia katika usiku wa siku hiyo, hivyo
miale ya jua ilikuwa imeshapoteza ubora wake, na kuleta nuru hafifu, na
kuifanya kuwa jioni ya siku hiyo. Ni nyakati hizo ambazo maongezi ya mama na
mjomba hayakuwa na uhai tena, baada ya kuagana hatimaye tulishika njia kutoka
nyumbani kuelekea kilipo kituo cha daladala, ambazo zingemuezesha mjomba kufika
nyumbani kwake kutokea mahali pale. Kituo cha daladala nacho hakikuwa karibu
sana, kiasi kwamba ndio ilikuwa njia ya mimi kuweza kunipatia majibu ya maswali
pindi ambapo nilipokuwa nayahitaji.
Nilimuangalia mjomba katika jicho la
kuibia ibia lakini bado alionekana hayuko sawa, mtazamo wake ulionekana kubabea
mambo mengi ambayo yanamsumbua katika namna moja ama nyingine, akili yangu muda
huo ilikuwa ikipambana na juu ya kuuliza kile kilichokuwa ndani yangu, nilipima
uzito wa lile jambo, uthubutu wa kuuliza ukanipotea huku nikikabwa kabisa,
wakati huo ukimya ukitutawala miongoni mwetu baada ya maogezi machache ya hapo
awali wakati tunatoka.
_______
Sikuwa mtu wa kupenda kushindwa
nilipokumbuka kuwa sipendi kitu kinachoitwa kushindwa jambo. Haki nilijikaza na
kuufukuza ukimya katika namna ambayo mjomba hakuitegemea. Swali zito lilinitoka
na kumwelekeza mjomba katika hali ya kizembe mno ya kuuliza, swali ambalo
sikutegemea uwenda ningepokea majibu katika hali isiyozuilika.
Kiukweli kilio cha mjomba hakikuwa
mbali, alilia sana. Kilio ambacho kiliniumiza, si kupenda hali ile niliyokuwa
nikiiyona nilijitamani kujilaumu, lakini sikuwa namna njiani pale, ilininibidi
nigeuke mbembelezaji, niliitahidi kuzuia kilio chake, japo kwa muda kidogo
kabla ya kuendelea na safari.
Nikiwa sitegemei kama mjomba anaweza
kuniambia chochote, baada ya kunyamaza, hatimaye alianza kunijibu lile swali
langu niliokuwa nimeliuliza japo ilikuwa kwa ufupi isiyoleta tija kwa upande
wangu. “Ni kweli hatukuwahi kuwa na matatizo hapo nyuma na shangazi yako kama
ulivyoniuliza mpwa wangu, wewe ni bado mdogo sana, ujui jinsi maisha yalivyo
kimsingi kuoa uyaone”, alimaliza mjomba. Majibu ambayo yaliongeza tu maswali
upande wangu na kuleta mvutano wa kile nilichokuwa nikifikiri. Sikuwa na jinsi
kuhusu kukua niyaone ni kweli nilikuwa nimeshakuwa na tayari nilishaanza
kuyaona. Hivyo sikutaka kuendelea na udadisi sana.
Tuliendele kupiga hatua, bahati nzuri
tulikuwa tumeshasogea sana karibu na kituo cha daladala. Na hata macho yetu
yaliweza kukumbana na daladala ambazo nyingi zilikuwa zimejaza watu kuliko
kawaida. Tulipiga hatua chache, hatimaye pua zetu zilikumbana na harufu ya
kituo kile vizuri. Ilichukua muda kidogo katika uchaguzi wa daladala ambayo
ilikuwa walau ina nafasi ya kumwezesha mjomba kusimaa. Baada ya kufanikisha
hilo mimi niligueza kurudi nyumbani.
********
Giza nalo lilikuwa linaingia rasmi,
macho yangu yalishaanza kulipokea, ni nyakati ambazo nilikuwa, nimesharejea
nyumbani. Mama akiwa anajishughulisha kuandaa chakula cha jioni, nilimchombeza
kidogo katika hali ya kiutani, kama kawaida yangu. “Mama nawe” ilinitoka huku nikiweka mdekezo
wa kitoto, “mmh nini nawe ushaanza kudeka?” maneno ya mama ya kapenya kwenye
masikio yangu, katika hali ya kuuliza ambayo haikuwa ikihitaji majibu kwa
lazima. Tuliendelea kuzungumza kidogo. Maeneno yake ya kaleta furaja, upande
wangu nilijihisi mtu katika watu. Mama alikuwa akinifurahisha sana hata hali ya
unyonge kwa wakati mwingine ilikuwa ikinitoke, kutokana na vijimaneno maneno
vya mama kwa wakati fulani. Nilikuwa nikijisikia raha sana Mungu kunipa mama
kama yule.
Nilingia ndani, na kuketi sebuleni,
taratibu na kiendea runinga iliyokuwa ikiangaliana nami bila kuwa na uhai. Nikibonyeza
kitufe cha kuipa uhai, muda kidogo ilianza kubaliana na kile nilichokuwa
nataka, kukiweka nayo ikatii.
Masikio yangu yakanza kusikia sauti ya
runinga ile, huku macho ya kiona kile kilichomo ndani yake, ilikuwa ni nyimbo
za wasanii wetu wa hapa nchini. Hapo kidogo zilizidi kuniliwaza na kupoteza
fikra, ambazo zilikuwa zikinyanyasa kichwa changu. Muda nao haukuwa nyuma,
uliendelea kwenda, nyakati hizo hurufu nzuri ambazo zilikuwa zinatoka jikoni,
zilianza kunyanyasa pua yangu, huku tumbo nalo likiunguruma. Mama naye alishajua
kuwa mwanae sina hali hata kidogo, muda mchache nilimwona akija, lakini katika
namna nyingine.
********
Siku ya safari iliwadia hatimaye
mapema tuliacha ardhi ya Tanzania, wakati huo kabla ya hapo tuliingia katika
maombi mazito. Usiku wa kuamkia siku hiyo, maombi ambayo kwa upande moja ama mwingine
yalizidi kunipa faraja kuhusu hali yangu. Tulimuomba Mungu atuwezeshe kufika
salama ndani ya nchi ya India, na hata kuniwezesha afya yangu kuwa sawa.
Hatimaye Mungu aliweza kujibu maombi yetu japo hayakuwa yote, kwa pamoja.
Tuliweza kuingia India, baada ya masaa kadhaa angani ambayo sikuwa na uwakika
sana yalikuwa mangapi?.
Hali ya hewa haikuwa na tofauti sana
na nchini Tanzania kwa wakati ule, hivyo hakunisumbua kwa upande wangu, pia na
mama. Tulikumbana na tabu pale uwanja wa ndege lakini tuliweza kufanikiwa kumpata
mtu ambaye alikuwa anajua lugha ya kingereza. Hivyo iliweza kutusaidia kufanya
mawasiliano, hii ilitokana na wenyeji wengi wa nchi ya India hawakuwa na
kifahamu kingereza, hata Kiswahili ambazo ndizo lugha tulizokuwa tukizifahamu
mimi na mama.
Baada ya kufanikiwa kumpata dereva
moja wa tesi pale uwanja wa ndege ambaye alikuwa akijiua kingereza vizuri,
ilikuwa msaada mkubwa sana kwetu. Aliweza kutusaidia sana kuanzia siku ile ya
kwanza hadi siku ya pili tulipoelekea hospitali, ambayo haikuwa mbali na sehemu
ile tulipokuwa tumefikia.
Siku hiyo ilianza ya kupendeza sana
machoni mwetu, mwanga wa jua ulipenya ndani ya macho yetu na kuonesha fahari
yake, hata kunifanya kuachia tabasamu ambalo ilikuwa nadra sana kwangu kuachia
katika kipindi kama kile, tabasamu ambalo mwisho lilikuja kuchukizwa na siku
ile iliyoanza katika, mnang’aro wa kupendeza na kuleta tumaini kwa upande wangu,
hakika ilikuwa kama inanikebehi.
Post a Comment