Mechi ya Kwanza ilikuwa kati ya Kitumbikwela dhidi ya Mitandi ambayo mechi hiyo ilichezwa mnamo saa Nane mchana kama ilivyo ada.
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Mitandi kilichocheza dhidi ya timu ya Kitumbikwela.
Dakika 14 baadae ni Maulidi Manyanya aliipatia timu yake ya Mitandi bao la pili.
Richard Edgar aliweza kuifungia goli la Kufutia machozi timu yake ya Kitumbikwela mnamo dakika ya 26. Hadi kipindi cha Kwanza kinamalizika Matokeo yalikuwa 2-1.
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Mitandi kilichocheza dhidi ya timu ya Kitumbikwela.
Kipindi cha Pili kilianza kwa kufanya mabadiliko kwa timu zote mbili lakini bado timu ya Kitumbikwela ilionekana kuzidiwa na dakika ya 51 Hassani saidi aliweza kuifungia goli la 3 timu yake hiyo, Dakika ya 64 Peter jololo alifunga goli la 4 huku goli la tano na la Ushindi liifungwa na Hassani Saidi tena na kuweza Kufunga Hattrick ya Kwanza katika Michuano hiyo.
Hadi Kipyenga cha mwisho matokeo yalisoeka Kitumbikwela 1 - Mitanda 5
Timu zikiingia Uwanjani: Kata ya Makonde dhidi ya Mikumbi.
Mnamo Saa Kumi za Jioni Timu ya Kata ya Makonde iliweza kuiadhibu timu ya Kata ya Mikumbi kwa kuifunga magoli 5 - 0 japo Mikumbi waliweza kupata nafasi ya Penalt na kushindwa kuitumia.
Magoli ya Makonde yalifungwa na Juma Kado (dak 10, 33, 69), Mohamed Hamis (dak 24 Penalt), Muksin Rashid (dak 52),
Timu zikisalimiana Kabla ya Mchezo kati ya Makonde dhidi ya Mikumbi.
Leo julai 18 mashindano hayo yataendelea kwa Kuzikutanisha Timu ya Maafisa wa Polisi Vs Kata ya Matopeni.
Post a Comment