Profesa Janabi, ambaye pia ni daktari Mkuu Binafsi wa Rais Mstafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alikuwa akikaimu nafasi hiyo toka kuanza rasmi kwa taasisi hiyo Septemba 2015 na inayoendelea kujizolea sifa kwa huduma zake za moyo ambazo awali zilipatikana nje ya nchi. Tasisi hiyo hivi sasa inajitegemea.
Taasisi ya Jakaya Kikwete inatoa matibabu pamoja na mafunzo ya Ubingwa wa juu katika fani ya Upasuaji wa Moyo , Usingizi na Tiba ya Moyo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili( MUHAS) na taasisi za moyo mbalimbali duniani.
Profesa Janabi ni mmoja kati ya viongozi na watendaji wa taasisi mbalimbali za serikali ambao waliteuliwa kushika nyadhifa July 16, 2016 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Wengine walioteuliwa ni Mhe. Augustino Lyatonga Mrema ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole, Prof. William R. Mahalu aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na Prof. Angelo Mtitu Mapunda ambaye ameteuliwa kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kwa kipindi cha miaka mitatu. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Wengine walioteuliwa ni Sengiro Mulebya (Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama), Oliva Joseph Mhaiki (Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Winifrida Gaspar Rutaindurwa (Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Charles Rukiko Majinge (Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili) na Dkt. Julius David Mwaiselage ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Uteuzi huu umeanza tarehe 15 Julai, 2016.
Post a Comment