0



Leo kulikuwa na mcheza wa jadi huku kila timu ikicheza kufa na kupona kuweza kusaka ushindi lakini wote walitii sheria bila shuruti
Baki wa timu ya Transporter Abdalahi Badi akiwa amebebwa na kutolewa nje baada ya kuchezewa rafu

Mchezaji wa timu ya Transporter Saidi Milasi akiwa amebebwa mara baada ya kuchezewa rafu na mchezaji wa timu ya polisi fc


Ligi ya Liwale super cup leo julai 6 kulikuwa na mchezo wa watani wa jadi uwanja wa wilaya ya Liwale kati ya POLISI FC Vs TRANSPORTER FC.
Katika kipindi cha kwanza timu zote zilicheza mpira kwa kasi huku kila timu ikiwa inatafuta magoli ya kuongozi ili kuweza kuweka historia ya mchezo wa leo lakini jitihada na mbinu zilifanana na kulazimika kipindi cha kwanza kufungana magoli 2 kwa 2 katika dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza.
Magoli ya polisi fc yalifungwa na SHWANGWE SHANGWE dakika ya 33 na GOLI LA PILI TRANSPORTER WALIJIFUNGA WENYEWE KWENYE HARAKATI YA KUOKOA Kupitia kwa baki wao ABDALAHI BADI katika dakika ya 37.

Magoli ya timu ya TRANSPORTER FC  yalifungwa na Shabani Mbwani Dakika ya 6 na Saidi Milasi dakika ya 39.

 na Matokeo mpaka dakika 90 zinakamilika ilikuwa SARE YA 2 KWA 2.

Kocha wa timu ya Transporter fc Ridhiki Mbwani alisema mchezo wa leo ulikuwa mgumu upande wake na kulazimika kutoka sare lakini anajipanga upya kwa mechi ijayo ili kuweza kuibuka na ushindi nae kocha wa Polisi fc Josepherter  Kubeleka aliweza kuzungumzia mchezo wa leo na kusema timu yake kila siku ikicheza kwao ni ligi na kusaka ushindi na hatarajii kupoteza mcheza hata mmoja na amewaomba mashabiki wa soka kuweza kuisapoti timu ya polisi fc.

Post a Comment

 
Top