Mbunge wa jimbo la Liwale,mh.Zuberi Kuchauka wa pili kutoka kushoto akishiriki swala ya Eid iliyoswaliwa leo kiwilaya ilifanyika katika kijiji cha Makata kata ya Makata wilayani Liwale
waumini wa dini ya kiislamu wakiwa kwenye swala ya Eid iliyoswaliwa leo kiwilaya ilifanyika katika kijiji cha Makata kata ya Makata wilayani Liwale
Mbunge wa jimbo la Liwale Zubeir Kuchauka (CUF),amewataka waumini wa
Kiislamu kuendeleza yale mema waliyokuwa wakifanya katika kipindi cha
mwezi mtukufu wa Ramadhani .
Alisema hayo leo wakati wa swala ya Eid kiwilaya iliyofanyika katika Kijiji cha Makata Kata ya Makata wilayani Liwale mkoani Lindi.
Alisema kama kuna jambo jema alilofanya muislamu ni
kufunga na sala alizokua akifanya hivyo mema hayo yaendelee na si
kujiingiza katika maasi.
Aliwataka waumini wote wa kiislamu na wale wasio waislamu
kuungana pamoja katika kusherehekea sikukuu ya Eid ambayo inabaraka kwa
kila mmoja.
Naye Sheikh Mkuu wa Wilaya Adam Mpelengano alisema
aliwataka wananchi waislamu wote kuweka siasa kando na badala yake
kufanya kazi pamoja na kushirikiana katika kila jambo.
Imamu wa msikiti huo wa Makata Sheikh Issa Muage alisema
siku ya Leo( jana)ndio siku ya Takbir kwa kila mtu kuendelea na toba na
haifai kurudi katika maasi.
"Si tena kurudia madhambi baada ya kutubu na isiwe leo
sikukuu ukaitumia vibaya kwa kufanya maovu basi funga yako yote utakua
insights,"alisema Sheikh Muage.
Alisema kwa aliyefunga Ramadhani hii ni sawa na mtu
aliyefunga mwaka mzima na kuwataka waislamu kuendelea na kupata thawabu
kwa kutoa dhaka kwa watu wasio jiweza.
Post a Comment