MBUNGE wa Jimbo la Liwale, Zuberi Kuchauka (CUF) ameeleza sababu ambazo zilimfanya asiingie ukumbini katika Bunge lililopita la bajeti lililoisha hivi karibuni mjini Dodoma.
Hayo aliyaeleza jana katika mkutano wa pili maalum na wazaliwa wa Wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambao wanaishi jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Chuo cha Bandari, Temeke ambao walimtaka mbunge huyo asijihusishe na migomo ambayo aina tija kwa Wanaliwale.
Alisema alishindwa kuingia katika vikao hivyo kutokana na maamuzi yao ya wabunge wa Ukawa kutokana na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Ackson Tulia alikuwa anashindwa kuwapa nafasi wapinzani.
Kuchauka, alizidi kufafanua kuwa hawezi kukaa bungeni wakati viongozi wa juu wa chama hicho wametoa maamuzi ya kugomea bunge hilo ambalo walinyimwa haki zao za kikatiba.
"Ndugu zangu mimi nisingeweza kutoka nje maana maamuzi ambayo tuliyochukua yalikuwa ya wote wabunge wa Ukawa, pamoja na uongozi wa juu na lengo letu sisi kurudisha heshima ya bunge baada ya kuona Naibu Spika wa Bunge, Dk. Ackson Tulia alikuwa anatunyima haki zetu na kuzipuuzia hoja zetu.
"Mimi naumia na nyinyi, msione kama sina machungu ukiangalia kabla ya Spika wa Bunge, Job Ndugai kuumwa nilikuwa nimechangia mara tisa, na nilikuwa naisemea Liwale ambayo imesaulika, ila leo tumekuwa tunanyanyasika ndio tukafikia hatua hii ya kutoka nje," alisema Kuchauka.
Alisema kwa sasa atatumia njia mbadala ya kusikilizwa hoja zake za shida ambazo zimekuwa sugu jimbni kwake ili kufikia mafanikio.
Aidha, alisema kuwa katika kuyafanyia kazi mambo ambayo aliyalilia bungeni, Waziri wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe atatembelea jimboni humo kuangalia fursa za kiutalii kwenye Hifadhi ya Wanayama ya Selous.
Kuchauka aliwataka wakazi hao ambao wenye uwezo kwenda kuwekeza nyumbani kwao ili waweze kutumia rasilimali ambazo zinapatikana jimboni humo.
Pia, wakazi wamepanga kufanya harambee ya kuchangia kupata Sh. milioni 83 ambazo zitawesha kupatikana redio ambayo itakuwa chini ya Halmashauri ya wilaya hiyo.
KUANGALIA PICHA ZA KWENYE MKUTANO MAALUM BOFYA >>HAPA
KUANGALIA PICHA ZA KWENYE MKUTANO MAALUM BOFYA >>HAPA
Post a Comment