Kaimu mwenyekiti wa halmashauri
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya
Liwale , Justine Monko akiwa anatoa ufafanuzi kuhusiana na mambo mbalimbali kwenye baraza la madiwani
LIWALE, BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya
Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi limeridhia kufutwa kwa mkataba wa
Kampuni ya JHS kwa kushindwa kumaliza kazi kwa muda mwafaka .
Maamuzi hayo yalifanyika Julai 27 katika
Kikao cha mwaka cha baraza la madiwani lililofanyika ukumbi wa Halmashauri, huku madiwa wakidai
kampuni hiyo imeshindwa kufanya kazi
kwa wati hivyo inaweza kuisababishia
halmashauri hasara kubwa.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya
Liwale , Justine Monko alisema ipo haja ya
kufuta mkataba na kampuni ya JHS
kufanya kazi na Halmashauri kwakuwa
kampuni hiyo imeshindwa kufanya kazi
katika muda mwafaka huku akisena dawa
ya jipu ni kulitumbua.
Pia, baraza hilo liliazimia kumsimamisha
kazi mwandisi wa ujenzi wa halmashauri
kwa kushindwa kusimamia baadhi ya
miundombinu ya barabara zilizopokelewa
huku zikiwa zimejengwa chini ya kiwango Licha ya madiwani wa kata ya Liwale mjini
kukataa barabara hizi kwa kujengwa chini
ya kiwango.
Hata hivyo baraza liliamua na kumpa onyo kali ya mwisho mwandisi huyo kwa kumwambia anatakiwa kufuatilia kwa ukaribu na kwa umakini kuanzia sasa.
Hata hivyo baraza liliamua na kumpa onyo kali ya mwisho mwandisi huyo kwa kumwambia anatakiwa kufuatilia kwa ukaribu na kwa umakini kuanzia sasa.
Diwani wa kata ya Nangando,Jafari
Mkungu alisema kwenye kata yake kuna barabara ya mita 400 ya Kambarage
iliyopo katika kijiji cha Mbonde kata ya
Nangando ambayo imejengwa chini ya
kiwango nae diwani wa kata ya Liwale
mjini Adamu Mahekula aliikaa kuipokea
barabara ya mita 850 ambayo ya kutoka
kwa tengeneza hall mpaka kwa msikiti wa
Mbinga iliyojengwa chini ya kiwango pia.
Baraza lililalamikia kuwepo kwa madawati
yasiyo na kiwango hiyo wameitaka
halmashauri kuhakikisha mkandarasi
aliopewa tenda hiyo kutolipwa kwanza
pesa mpaka pale ayafanyie marekebisho
madawati yote yaliotengewezwa chini ya
kiwango kwa ghalama yake.
Diwani wa viti maalu,Siwema Mbogo
waliwatupia lawama wakuu wa idara kwa
kushindwa kutoa taarifa zao kwa umakini
hiyo amewata wakuu hao wa idara wawe
makini katika utoaji wa taarifa zao hatua
hii ilifikia baada ya kuwepo taarifa mbili
tofauti za kuwepo idadi sahihi ya
madawati katika shule ya msingi
Tepetepe.
Katika baraza hilo katika halmashauri ya
wilaya inaonesha hakuna watumishi hewa
lakini mkurugenzi wa halmashauri,Justine
Monko hawezi kuipeleka
yake kwenye kisu hivyo alisema zoezi la
uhakiki wa watumishi hewa litarudiwa
tena ili kuweza kujirizisha richa ya ofisi
yake kukuta taarifa ya watumishi hewa 0.
Post a Comment