0


 Mchezaji wa timu ya Kigamboni fc akijaribu kuangalia kwa kugawa pasi waweze kufunga
 Wachezaji wa timu ya Hawili fc ikishangilia goli mara baada ya kufunga
 Mchezaji wa Hawili fc akijipanga tayri kwa kupiga mkwaju wa penaiti
 Golikipa wa timu ya Hawili fc akijipanga tayari kwa mikwaju ya penaiti

Hatua ya Robo fainali ligi ya Liwale super cup imeendelea tena leo julai 13 mchezo uliochezwa uwanja wa wilaya ya Liwale kulikuwa na mchezo mmoja kati ya Hawili fc dhidi ya Kigamboni fc.

Katika kipindi cha kwanza hadi dakika 45 zinamalizika hakuna timu hata mmoja ilioweza kufumania nyavu ya mwezake.

Baada ya mapumziko Kipindi cha pili namo dakika ya 55 Laurensi Fusi aliweza kuiandikia timu yake ya Hawili fc. 
Hadamu Kandimwa mchezaji wa Kigamboni fc katika harakati ya kutaka kuokoa mpira goli kwake aliweza kujifunga mwenyewe namo dakika ya 61.

Dakika ya 63 Rehmani Mtipa aliweza kupachika goli na dakika ya 77 Rehmani Mtipa aliweza kusawazisha na kupelekea mpaka dakika 90 zinakamilika ikawa sare ya magoli 2 kwa 2.
 
Mwamuzi wa mchezo akaamua kupigwa kwa mikwaju ya penaiti,timu ya Hawili ilikuwa ya kwanza kupiga penaiti.
 
Hawili fc waliweza kupiga penaiti 5 wakakosa moja 4/5 nao Kigamboni  fc waliweza kupiga penaiti 5 wakakosa moja 4/5.
 
Zikaamuliwa zipingwe zingine wakaanza kupiga Hawili fc wakakosa na Kigamboni fc ikawa zamu ya Rehmani Mtipa aliweza kutikisa nyavu na kuifanya Kigamboni kuingia katika hatua ya nusu fainali.
 Makotokeo yakawa Hawili 6-7 Kigamboni fc.

Julai 14  kutakuwa na mchezo mkali tena utakaowakutanisha TRANSPORTER Vs NANGANDO FC mchezo utaochezwa kwenye uwanja wa wilaya ya Liwale majira ya saa 10 jioni.

Post a Comment

 
Top