0


Kocha mpya wa Manchester City Pep Guardiola amesema kwamba ameamua kuja Ligi Kuu ya England ili kuthibitisha ubora wake

Jana idadi ya mashabiki takriban 7,000 walijitokeza kwenye uwanja wa Etihad Stadium kumsikiliza Guardiola akiongea kwa mara ya kwanza kama meneja wa Manchester City.

“Ndio maana nipo hapa. Nimethibitisha ubora wangu nikiwa na Barcelona, nimefanya hivyo nikiwa Ujerumani na Bayern Munich na sasa nataka kuthibitisha na England.” Guardiola amesema.

Siwezi kufanikisha hilo peke yangu. Nahitaji wachezaji, viongozi. Tunahitaji mashabiki. Bila ya hayo yote, kamwe hatutafanikiwa.

Mhispania huyo amejiunga na City akitokea Bayern Munich ambapo kwa miaka mitatu aliyodumu klabuni hapo amewapa ubingwa wa Bundesliga mara tatu licha ya kushindwa kufika hata mara moja fainali ya Klabu Bingwa.

Hata hivyo, kiungo huyo wa zamani wa Uhispania alishinda kombe hilo mara mbili wakati akiwa na Barcelona

Anaamini kwamba ushirikiana bora na kujituma ndio siri kubwa ya mafanikio mwenye timu.

Napenda wachezaji ambao hawajifikirii wenyewe tu bali wanafikiria muda wote juu ya timu (Manchester City),” amesema Guardiola.

“Sisi sote tunafanya kazi hapa kwa ajili ya timu. Sababu kubwa ya kuwa hapa ni kufanya kila linalowezekana kuifanya klabu yetu iwe bora.”

“Sihitaji watu ambao wana fikra za kutaka klabu iwafanyie wao mambo. Sote tuko hapa kuifanya Manchester City kuwa klabu bora kuelekea miaka mitatu au minne ijayo.”

Aliongeza: “Moja ya sababu zilizopelekea mimi kuja Manchester City ni kuwa na ufahamu juu ya (Mkurugenzi wa Michezo) Txiki Begiristain namna anavyothamini uwepo wa wachezaji vijana kuanzia umri wa miaka 13, 14, 15, 16, 17 na kuendelea. Hawa wanakuwa kwenye misingi ya timu na baadaye kuungana na sisi kwenye kikosi cha wakubwa.”

Post a Comment

 
Top