0

MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga,Godwin Gondwe  amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanawekeza kwenye kilimo kikubwa cha kisasa ambacho kitakuwa na tija kwao ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo na kukuza uchumi.
Gondwe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na  wafanyabiashara, viongozi wa dini ambapo pamoja na mambo mengine  aliwataka kuona umuhimu wa kutumia fursa ya uwepo wa rutuba nzuri ya ardhi iliyopo wilayani humo kujikita kulima kisasa ili kuweza kupata 
mafanikio.
Alisema kuwa lazima wafanyabiashara watambue kuwa kilimo ndio njia pekee  ambayo inaweza kuwainua kiuchumi na kuharakisha kasi ya ukuaji wa  maendeleo iwapo watazingati na kukipa kipaumbele kila wakati

  “Niwaombeni suala la kilimo mlipe  msukumo mkubwa sana  kwani hii ndio
njia pekee ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wilaya yetu “Alisema.
Aidha pia alisisitiza umuhimu wa wananchi wa wilaya hiyo kutilia mkazo 
kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwemo Alizeti, Ufuta,Viazi na
Mihogo ili kuweza kukabiliana na tatizo la kutoku patikana mvua za 
uhakika kwa ajili ya kilimo cha mahindi.
 “ Ninajua katika kipindi hiki tumelima kwa wingi lakini hali ya hewa 
sio nzuri na mvua nazo zimekuwa hazipatikana kwa uhakika hivyo lazima 
wakulima tubadilike kwa kuanza kupanda mazao yanayostahimili ukame ili 
kuweza kuepukana na baa la njaa “Alisema DC Gondwe.
Sambamba na hayo,Mkuu huyo wa wilaya alizishauri taasisi za kibenki 
wilayani humo kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa wawekezaji wa kilimo 
ili waweze kuzalisha kwa wingi mazao ambayo yataweze kuinua kiuchumi 
lakini pia kuchangia pato la Taifa. Hata hivyo ,Mkuu huyo wa wilaya alitumia pia fursa hiyo  
kuwaasa 
wakulima waliopata mazao kidogo kuhakikisha wanayatunza na kuacha  
kuyauza kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha hali ya njaa 
kwao

Naye Sherhe wa wilaya ya Handeni, Shabani Mohamed alisema kuwa wao
watamuombea dua Mkuu huyo wa wilaya ili mungu amuwezeshe kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo na kusaidia kuchangia juhudi za maendeleo kwa  wananchi.
 “Nikuambie Mh Mkuu wa wilaya ujio wako hapa Handeni watu wengi 
wamefurahi sana kwani uchapakazi wako unafahamika tokea ulipokuwa 
unafanya kazi kwenye kituo cha ITV na tunaamini uhodari huo pia 
utasaidia kuinua uchumi wetu “Alisema.

Alisema kuwa wao watahakisha wanampa ushirikiano wa hali ya juu ili
kumuwezesha kutekeleza vema majukumu yake ya kuipa maendeleo wilaya
hiyo.

Post a Comment

 
Top