0
Mafuriko yaua watu Ulaya
Watu wanne walifariki Jumatano katika mafuriko yaliyokumba Ufaransa na Ujerumani.
Makundi ya uokoaji yaligundua maiti tatu katika mji wa Bavaria.
Waathiriwa walikwama nyumbani mwao wakati wa mafuriko hayo.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 86 alipatikana amefariki katikati mwa Ufaransa.
 
Watu wanne walifariki Jumatano katika mafuriko yaliyokumba Ufaransa na Ujerumani.
Miji kadhaa imekumbwa na mafuriko.
Waziri wa Mazingira wa Ufaransa, Segolene Royal, alijionea mwenyewe alipopaa kwa helikopta juu ya mji mmoja na kujionea jinsi mto Seine ulivyovunjika kingo zake.
Watabiri wa hali ya anga wanatarajia mafuriko mengine kutokana na mvua ambayo inatazamiwa siku kadhaa zijazo.

Post a Comment

 
Top