Viongozi wa nchi za
Magharibi mwa Afrika wamejadili mpango wa kuanzisha kikosi cha
kupambana na wapiganaji wa Ki-Islamu katika kanda hiyo.
Wapiganaji
wenye uhusiano na Al Qaeda wamefanya mashambulio nchini Mali, Ivory
Coast na Burkina Faso, na kundi la Boko Haram, mara kadha, linashambulia
maeneo ya Nigeria na nchi jirani.Viongozi hao wanaokutana mji mkuu wa Senegal, Dakar, hawakutoa maelezo kuhusu mpango huo.
Pia wametaka uchaguzi ujao wa Gambia uwe huru, na askari wa usalama wasitumie nguvu nyingi dhidi ya raia.
Post a Comment