Baadhi ya Bidhaa Ambazo zinazozalishwa na Vijana Wajasiriamali
Vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 25 wanaoishi katika mazingira magumu
na hatarishi wamepatiwa mafunzo ya ujasiliamali na jinsi ya kuendesha
biashara ambapo wanaenda kufungua mampuni mbili za kijasiliamali na
kuondokana utegemezi.Elimu hiyo imetolewa na Shirika la kazi duniani ILO kwa kushirikiana na taasisi ya Beila, huku vijana waliofuzu mafunzo hayo ya wiki moja wakiiomba serikali kuhakikisha kuwa inawaunga mkono katika shughuli zao kwa kuanza na kuwapa usajili mapema ili kuendelea na shughuli za uzalishaji.
Vijana hao kupitia Mwenyekiti wao Isaya Venance amesema kuwa wanaiomba serikali kuwasajili mapema kwa kuwa kumekuwa na vikundi vingi vinavyopatiwa mafunzo kama waliyoyapata lakini wanakwama katika usajili.
Aidha mkufunzi wa mafunzo hayo kwa vijana hao Dk. Edwin Mweleka amesema kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa ajili ya kuwainua vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuwainua kiuchumi na kuwasaidi kuepukana na kujiunga na makundi mabaya ya uhalifu na kuwa kupitia mafunzo ya aina hiyo yanaweza kuwasaidia vijana kuwa na ubunifu wa kibiashara.
Akifunga mafunzo hayo Diwana wa Kata ya Ramazani George Sanga amesema kuwa kikundi hicho atahakikisha kuwa kikundi hicho kinasajiliwa kwa wakati ndani ya wiki hii ili waanze kufanya kazi kwa kutumia ujuzi walio upata wakati wakipata mafunzo hayo.
Post a Comment