0


 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inawakumbusha walipakodi wote kulipa Kodi ya Mapato na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kabla ya tarehe 30 Juni 2016 ili kuepuka usumbufu na msongamano. 
TRA pia inawakumbusha wafanyabiashara wote wa Dar es Salaam ambao mauzo ghafi ni kati ya  shilingi millioni 14 na milioni 20 kwa mwaka kufika ofisi za TRA katika mikoa yao husika kuchukua mashine za EFDs kabla ya tarehe 30 Juni 2016. 
Baada ya tarehe 30 Juni, zoezi la kugawa bure mashine za EFDs katika mkoa wa Dar es Salaam litasitishwa.   
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja simu namba: 0800750075 au 0800780080 
Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
Mamlaka ya Mapato Tanzania
Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top