Mchezaji wa timu ya Super Star kutoka kijiji cha Mihumo jezi nyeusi akisakata mpira leo kwenye uwanja wa wilaya ya liwale
Ligi ya Liwale Super Cup inayoendelea hapa wilayani leo june 27 kulikuwa na mchezo wa aina yake mchezo uliotimua vumbi katika uwanja wa wilaya kati ya Super star Vs Nangando fc na kupelekea kutoana jasho ya sare ya goli 3 kwa 3.
Timu ya Nangando fc ndio ilikuwa ya kwanza kujipatia goli namo dakika ya 10 lililofungwa na Yuba Mmocha na Super star walisawazisha dakika ya 17 kupitia mchezaji wao Juma Ngokwe lakini Nangando fc wajipatia goli la pili dakika 45 kabla ya mapumzika goli lililofungwa na Yuba Mmocha.
Katika kipindi cha pili dakika ya 47 Imamu Katundi aliindikia Nangando fc goli la tatu lakini Super star waliweza kusawazisha katika dakika ya 65 goli likifungwa na Juma Ngokwe na goli la tatu kifungwa na Pani Malinga katika dakika ya lala salama dakika ya 80.
Toka ligi ianze leo ni mara ya kwanza kwa timu kutoka sare ya goli 3 kwa 3 huku kocha wa Nangando Issa Kihaku alisema mchezo wa leo upande wao ulikuwa mzuri nae kocha wa Super star Saidi Mkungura alisema mchezo ulikuwa mzuri japo kulikuwa na kasoro ndogondogo lakini atajitahidi kuyarekebisha ili mechi ijayo aweze kupata ushindi mnono.
Post a Comment