0
Diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga Emmanuel
Siku moja baada ya kutokea kwa tukio la Makaburi Kufukuliwa na wanyama aina ya Fisi,Diwani wa Kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga  Emmanuel Ntobi(Chadema) ametoa kauli kuhusu tukio hilo..Soma Hapa Chini

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kuwepo kwa Tukio la kufukuliwa Miili ya Ndugu zetu, waliozikwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, katika Makaburi ya Mageuzi -Ngokolo, maarufu Makaburi ya Dodoma.

Maiti hao walizikwa na Manispaa yetu ya Shinyanga. Kwamba, 01 June 2016, walifukuliwa na Fisi na Mbwa katika Makaburi hayo.

Miili hiyo ilionekana kuliwa na Wanyama hao usiku, sehemu za miili na mifupa ya binadamu hao, ilizagaa katika mitaa ya Mageuzi, Ndembezi na Mwadui.


TUKIO HILI LINAVUJA KATIBA YA NCHI NA UTU WA UBINADAMU.

Tukio hili la kusikitisha, lilalovua utu wa ubinadamu na Katiba ya Nchi

kwa mujibu wa HAKI ya kikatiba Ibara ya 16 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 kila mtu ana HAKI ya kikatiba ya kuthamini utu wake kuwa faragha akiwa hai au amefariki.

Kwamba, Mtu yoyote anasitahili kuheshimiwa hata baada ya umauti kumkuta, anasitahili kuhifadhiwa kwa heshimika kwa kuzingatia Mila, Desturi na Utamaduni wetu wa Kitanzania.

NINI CHANZO CHA TUKIO HILI.
Chanzo cha tukio hili la kusikitika, Si hao fisi wala Mbwa, HAPANA. ni Uzembe na Kutokuwajibika kwa Watendaji wetu wa Manispaa ya Shinyanga.

Watumishi hawa, walichimba kaburi fupi sana, wakavunja mila na desturi zetu za kuchimba kimo kirefu ili waweze kuwahifadhi hao ndugu zetu.

NINI KIFANYIKE.

Mosi, Ndugu zangu, kwa kuzingatia hali hiyo, ninawaomba tushirikiane kulaani vikali tukio hili kwa nguvu zetu zote.

Pili. Wahusika wote wa kadhia hii, wachakuliwe hatua kali za kinidhamu na kisheria. Ili iwe fundisho na kwa wengine.

Tatu, Tumtake Mkurugenzi wa Manispaa yetu, ajipime kama anaweza kuendelea kututumikia kwa kuvunja katiba. Na kwa kushindwa kwake kuwajibika.

Mwisho, Mpaka sasa si Mkurugenzi wala vyombo vyovyote wilaya/ Mkoa, vimechukua hatua dhidi ya tukio hilo. Tuwape siku 7. Wakishindwa Tuchukueni hatua sisi wenyewe.
Asanteni

Emmanuel Ntobi
Diwani kata ya Ngokolo

Post a Comment

 
Top