MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu
amewekwa rumande kwa kukosa dhamana, mara baada ya mahojiano na Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kufuatia kauli yake aliyoitoa jana
inayoelezwa kuwa si ya kuingwana.
Kukosa dhamana hiyo kunafuatia kwa Mbunge Lissu kuripoti katika kituo cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa na Jeshi hilo kuhusu kauli yake aliyoitoa jana baada ya kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mbunge huyo amehojiwa kwa saa tatu kuhusiana na maneno mengine ambayo anayodaiwa kuyaandika kupitia mitandao ya kijamii kuwa ni ya uchochezi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amekili kuwa Lissu amewekwa rumande kwa kukosa dhamana na hataachiwa leo, hivyo atalala huko mpaka kesho.

Post a Comment