Mohamed Kuno aliuawa pamoja na watu
wengine wanne na maafisa wa usalama Kusini mwa Somalia.
Serikali ya Kenya inasema kuwa Kuno
ndiye aliyepanga mauaji ya chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 148 na
wapiganaji kutoka kwa kundi la wapiganaji kutoka Somalia al-Shabab.
Kuno,ambaye ni raia wa
Kenya alielekea Somalia na pia alilaumiwa kwa mashambulio kadhaa ya kikosi cha
wanajeshi wa Kenya wanaokabiliana na al-Shabab.
Serikali ya Kenya ilitoa zawadi ya zaidi
ya dola 200,000 kwa mtu atakayemkamata kufuatia shambulio hilo la Garissa.
Post a Comment