Polisi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria wamempata msanii maarufu ,Ado Daukaka,aliyepotea siku ya Ijumaa.
Wanasema wamemkuta akiwa katika hali ya kutokuwa na fahamu huku akiwa amekonda sana.
Daukaka
ameiambia BBC kuwa alitekwa nyara na kundi la watu waliokuwa na hasira
kutokana na wimbo aliouandika uliokuwa unawazungumzia viongozi wa siasa
wanajihusisha na rushwa.
Amesema walimuweka ndani kwa siku mbili bila ya kumpatia chakula na kisha kumtelekeza msituni.
Kwa sasa anaendelea na matibabu katika hospitali moja iliyopo kilomita 120 kutoka eneo alilotekwa.
Mojawapo
ya nyimbo zake ni unaoitwa kwa lugha ya Kihausa Gyara kayanka,
ukimaanisha ''tunapaswa kufanya matendo mema'' unaowazungumzia wanasiasa
wanaotoa ahadi nzuri bila kuzitimiza.
Post a Comment