0


Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Kamishna msaidizi wa polisi Leonard Paul amesema Jeshi la polisi limefanikiwa kumuua mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi sugu Benjamini Wallace Singano aliyekuwa na silaha ya kivita aina ya AK. 47.

Bunduki hiyo ilikuwa na magazini mbili zinazoingia kila moja wapo risasi 30 na mtu huyo ameuawa kwa kupigwa risasi wakati alipokuwa akijaribu kuwatoroka askari polisi,mara baada ya kukamatwa na kuelezea kuwa yeye na wenzake walikuwa wakienda kufanya uhalifu.

Kamanda Leonard amesema jambazi huyo alikuwa na silaha yenye namba 1678 MJ 0736 aliyokuwa ameificha katika begi dogo mithili ya mtu anayesafiri amekamatwa katika eneo la chekelei lililopo wilayani Korogwe katika barabara kuu inayounganisha mikoa ya Arusha tanga kwenda jijini Dar es Salaam.

Kufuatia hatua hiyo Kamanda paul amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kufanikisha vitendo vya uhalifu kwa kuwafichua watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kwa sababu silaha ya aina hiyo endapo ingeendelea kuwa mikononi mwa wahalifu ingeweza kusababisha maafa makubwa na hasara ya mali za watanzania.

Post a Comment

 
Top