0

Ligi Kuu ya England ndiyo yenye mvuto mkubwa zaidi katika soka duniani, na sasa imefikisha miaka 20 tangu ilipoanza.

Ligi hii ilianzishwa na Chama cha Soka cha England Februari 20, 1992 kutokana na uamuzi wa klabu kuachana na Ligi ya Soka iliyoasisiwa 1888.

Kwa kuachana na ligi hiyo ya zamani na kuanzisha Premier League, klabu hizo ziliingia kwenye mikataba minono na haki za kuoneshwa kwenye vituo vya televisheni.

Hadi kati ya mwaka 2008 na 2009, thamani yake ilikuwa Pauni bilioni mbili. Hii ndiyo ligi ya soka inayotazamwa nawatu wengi zaidi duniani, ikirushwa kwenye nchi takriban 212 na watazamani milioni 643.

Katika msimu wa 2010/2011 wastani wa mahudhurio kwenye kila mechi ya Ligi Kuu ulikuwa watu 35,363 na ujazo uwanjani ulikuwa asilimia 92.2.

Ligi Kuu ya England imeshika nafasi ya kwanza katika Umoja wa Vyama vya Soka vya Ulaya (UEFA) katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, ikizipiku hata zile ligi kubwa kama ya Hispania – La Liga na Bundesliga ya Ujerumani.

Tukirudi kwenye ligi ya awali, tangu 1888 klabu 23 za soka zimevishwa taji la soka la England. Kati ya klabu 45 zilizoshindana tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu mwaka 1992, nne zimetwaa kombe hilo, nazo ni:-

Manchester United iliyonyakua mataji 12, Arsenal mara tatu sawa na Chelsea, huku Blackburn Rovers ikiliambulia mara moja.
Wengi wanasema soka ni magoli, hivyo wafungaji magoli wametokea kuwa watu wanaoshangilia sana, na pengine kuhamishwa kwa kitita kikubwa msimu wa usajili unapojiri.

Cech amekuwa chaguo la pili kwenye klabu ya Chelsea ,huku mbelgiji Thibaut Courtois (kulia) akichukuwa namba !
Cech amekuwa chaguo la pili kwenye klabu ya Chelsea ,huku mbelgiji Thibaut Courtois (kulia) akichukuwa namba !
Ndiyo kusema wengi wao pia wamekuwa wakilipwa kiasi kikubwa cha fedha, na ndio wenye majina makubwa zaidi pia.
Katika miaka hii 20 ya Ligi Kuu, wapo waliopachika zaidi ya mabao 100, na wanaoshikilia rekodi ya juu zaidi wameshastaafu soka, ambapo wanaoendelea kuisakata hawajafanikiwa kuvunja rekodi hiyo.

Anayeongoza hadi sasa ni Alan Shearer aliyepindukia kwa mbali rekodi ya mabao 100 na kufikisha 260 hadi kutunukiwa Nishani ya Heshima ya Ufalme wa Uingereza (OBE).

Huyu alizaliwa Agosti 13, 1970 na alianzia soka kwenye klabu ya Southampton, akapanda chati na kuwa mfungaji mahiri alipojiunga na Blackburn na kumalizia ngwe yake ya soka akiwa na Newcastle.

Anakumbukwa kwa umahiri wake wa kunasa mipira ya juu kwa kichwa, lakini pia jinsi alivyokuwa tishia kwa mipira ya karibu na lango na ile iliyokufa akiipiga kutoka umbali wowote. Amepata kupewa hadhi ya mchezaji bora wamuongo na pia yumo kwenye orodha ya wachezaji mahiri 100 walio hai wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Aliichezea timu ya taifa ya England mara 63 na kufunga mabao 30 na amekuwa nahodha wake mara 34. Shearerkwa sasa ni mchambuzi wa masuala ya michezo, akishiriki na Kituo cha Televisheni cha BBC kwenye kipindi maarufu cha ‘Match of the Day’ kinachohusisha uchambuzi wa mechi ya siku husika. Huyu alipata kuwa kocha waNewcastle kwa muda kwenye msimu wa 2008/9 katika mechi nane za mwisho alipokuwa ameitwa kuokoa jahazi la klabu lililokuwa linazama kwa timu kushushwa daraja.

Andy Cole ndiye anashikilia nafasi ya pili kwa wingi wa mabao, akiwa ametia kimiani mabao 187. Akipenda zaidi kuitwa Andrew nyakati hizi, mshambuliaji huyo alizaliwa Oktoba 15, 1971 na alianzia soka yake ya umahiri na Arsenal, japokuwa alicheza hapo mechi moja tu kabla ya kuhamia Bristol City.

Umahiri wake katika upachikaji mabao ulimvutia kocha waNewcastle mwaka 1993, Kevin Keegan na kumsainisha kwenye klabu yake hiyo.
Katika hali ya utata, Cole alihamia Manchester United alikofikia kilele cha mafanikio yake akishirikiana na ‘pacha’ wake, Dwight Yorke.

Baada ya kuachana na Mashetani Wekundu hao, Cole alizichezea Blackburn, Fulham, Mancheser City, Portsmouth, Birmingham na Sunderland, pasipo kurejea kwenye kasi yake ya upachikaji mabao hadi alipostaafu 2008.

Washika Bunduki wa London, Arsenal, hawana ukame wa watu mahiri kwa miongo hii miwili kwenye Ligi Kuu, kwani Thierry Henry anayejifungamanisha na klabu hiyo bado, japo haichezei kwa sasa, amepachika mabao 176

Huyu alizaliwa Agosti 17, 1977 na alijiunga na Arsenal baada ya kucheza kwa mafanikio kiasi nchini mwake Ufaransa na Italia. Kocha wa Arsene Wenger ndiye aliyembadili Henry kuwa mfunga magoli mzuri na mabao yake yameipatia taji Arsenal mara mbili. Aliondoka Arsenal 2007 kujiunga na Barcelona ya Hispania kabla ya kuhamia New York Red Bulls na kurejea kwa hamasa Emirates Januari 2012, akiichezea Arsenal kwa mkopo kwa wiki saba na kufunga magoli muhimu machache.

Robbie Fowler aliyezaliwa Aprili 9, 1975 anashika nambanne kwa kufunga mabao 163 kwenye Ligi Kuu. Alikulia Toxteth, moja ya maeneo yasiyo na hadhi mjini Liverpool na baadaye akaja kuwa mmoja wa wachezaji mahiri wa timu ya mji huo, Liverpool.

Anakumbukwa zaidi kwa kipaji chake cha kumalizia mipira, ambapo katika hali isiyo ya kawaida, mwaka 1994 alifunga mabao matatu ndani ya dakika nne na sekunde 33, rekodi inayoshikilia hadi leo kwa ‘hat-trick’ ya haraka zaidi katika historia ya Ligi Kuu.

Aliondoka Liverpool kuhamia Leeds United na baadaye Manchester City, lakini alirejea dimba la Anfield kwa mwaka mmoja zaidi, msimu wa 2006/7. Baadaye alizichezea Cardiff City na Blackburn Rovers kabla ya kuhamia Australia mwaka 2009,alikocheza msimu mmoja katika klabu ya North Queensland Fury kisha kuhamia Perth Glory anakochezea hadi leo.

Les Ferdinand amefunga mabao 149 na alianza kung’aa kwenye upachikaji mabao akiwa na timu ya Hayes katika ligi za chini na kuendeleza ukali popote alipokwenda.

Alizidi kusikika baada ya kujiunga na Queens Park Rangers(QPR) alikochezea kwa miaka minane kabla ya kuhamia Newcastle United. Ferdinand akiwa na Shearer, walijenga ushirika tishio Tyneside na alionesha kasi, uimara na ukali wa aina yake mbele ya goli.

Miaka miwili baada ya kuwa Newcastle, Ferdinand alihamia Tittenham alikocheza kwamafanikio kipindi cha miaka sita kisha akaenda kuzichezea West Ham, Leicester, Bolton na Reading.

Michael Owen naye anashikilia rekodi ya mabao hayo hayo 149 kwenye Ligi Kuu. Huyu alizaliwa Desemba 14, 1979,na ni mwana wa mshambuliaji wa enzi za miaka ya ’70, Terry Owen.

Michael Owen alianzia Liverpool 1991kabla ya kuhamia Real Madrid mwaka 2004, na kurejea England msimu uliofuata baada ya kuwa akitumika kama mchezaji wa akiba huko Hispania. Baada ya kurudi alijiunga naNewcastle alikofunga magoli mengi kuliko idadi ya dakika alizocheza akiwa Hispania. Hadi msimu wa 2011/2 Owen ni mchezaji wa Manchester United.

Wachezaji wengine waliofunga zaidi ya mabao 100 nikiungo wa Chelsea, Frank Lampard aliyepata pia kuichezea West Ham United. Huyu ana mabao 149 wakati Teddy Sherringham aliyetamba na Notts Forrest, Tottenham Hotspur, Manchester United, Tottenham Hotspur, Portsmouth na West Ham alifunga mabao 147.

Wengine ni Wayne Rooney aliyepita Everton na sasa Manchester United mwenye mabao 134 na Jimmy Floyd Hasselbaink aliyeng’aa akiwa Leeds United, Chelsea na Middlesborough na kupata mabao 127.

Robbie Keane aliyechezea Coventry City, Leeds, Tottenham, Liverpool, Tottenham, West Ham na AstonVilla alizifuma nyavu mara 126.
Wafungaji mahiri wengine ni Dwight Yorke aliyeanziaAston Villa kabla ya kuhamia Manchester United, Blackburn Rovers, Birmingham City na Sunderland ambapo ana jumla ya mabao 123 huku Nicolas Anelkaaliyecheza Arsenal, Liverpool, Manchester City, Bolton Wanderers na Chelsea akiwa na mabao 123;

Ian Wright aliyeanzia kwa Washika Bunduki wa London na kisha kwenda West Ham amejilundikia mabao 113 wakatiEmile Heskey aliyekipiga Leicester, Liverpool, Birmingham, Wigan na Aston Villa akiwa na kumbukumbu ya mabao 111.

Dion Dublin aliyekipiga na Manchester United, Coventry na Aston Villa naye ana mabao 111 wakati Jermaine Defoealiyezichezea Tottenham, Portsmouth na West Ham akiwana mabao 109;

Ryan Giggs wa Manchester United amefunga 106 hukuPaul Scholes wa Mashetani Wekundu hao pia akiwa na mabao 103.
Gwiji Matthew Le Tissier (Southampton) amefunga mabao102 wakati Darren Bent aliyezichezea Charlton, Tottenham, Sunderland na Aston Villa akiwa na rekodi kamili ya mabao 100.

Kutokana na mvuto wa Ligi Kuu, takwimu zinaonyesha kwamba kuna wageni 750,000 kutoka nje ya nchi waliohudhuria mechi zake mwaka 2010, wakitumia jumla ya Pauni milioni 595.

Chagizo mojawapo kubwa kwa Ligi Kuu limekuwa kuibuka, kujijenga na kubakia kwa klabu zile ziitwazo ‘The Big Four’, yaani klabu nne kubwa ambazo miaka nenda rudi timu zake zimekuwa zikishika nafasi nne za juu.
Ukiiondoa Blackburn Rovers mwaka 1994-5, ni klabu tatu tu zimetwaa kombe la Ligi Kuu – Manchester United mara 12, Arsenal na Chelsea mara tatu kila moja.

Zaidi ya hapo, Manchester United haijapata kumaliza ligi nje ya nafasi tatu za juu tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu
Tangu msimu wa 1996-97 na kuendelea, ‘Top Four’ zimekuwa ni Arsenal, Chelsea, Liverpool and Manchester United zimetawala nafasi hizo kiasi cha kufuzu kwenye mashindano ya UEFA.

Awali ilikuwa klabu moja inafuzu, zikaongezwa kuwa mbili mwaka 1997, tatu mwaka 1999 na nne tangu 2002.
Faida za kufuzu, hasa ile ya ongezeko la mapato kwa klabu, zinaaminika kuongeza pengo kati ya timu hizo nne za juu na zile za chini.

Timu nyingine ambazo zimekuwa zikinyemelea kundi hilo la ‘Top Four’ ni Newcastle United na tangu 2009 timu mbili za Tottenham Hotspur na Manchester City zimekuwa zikipambana kupenya kwenye kundi hilo.
Kadhalika, timu zinazoshika nafasi za mwisho zimekuwana kawaida ya kuaibisha vinara wa ligi zinapokutana nazo, hasa katika michezo muhimu, vinara hao wanapohitaji ushindi.

Ligi Kuu hushirikisha klabu 20 na huendeshwa kwa mfumo wa michezo ya nyumbani na ugenini, ambapo timu inayohitimisha michezo yake kwa kushika nafasi ya kwanza ndiyo bingwa, wakati zinazoshika mkia hushuka daraja.

Msimu wake kwa kawaida ni kuanzia Agosti hadi Mei, timu zikicheza jumla ya mechi 38, ambapo mara nyingi mechi huchezwa Jumamosi na Jumapili na mara chache jioni ya siku za wiki.

Ligi hii ilianza kujulikana kama Premiership tangu 1993hadi 2007 na sasa inadhaminiwa na Benki ya Barclays, hivyo inatambulika rasmi kwa jina la Barclays Premier League.

Kumbukumbu ya Ligi ya Soka (iliyoshika nafasi ya Ligi Kuu kabla ya 1992) inaturudisha kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Aston Villa, Charlie Fossey aliyeshiriki kuianzisha.

Awali ilikuwa na daraja moja lenye timu 12 ambazo niAccrington, Aston Villa, Blackburn Rovers, Bolton Wanderers, Burnley, Derby County, Everton, Notts County, Preston North End, Stoke (sasa Stoke City), West Bromwich Albion na Wolverhampton Wanderers.
Ligi hiyo ilipokea wanachama zaidi mwaka 1892 kutoka kwa wapinzani waliojiita Football Alliance, ndipo ligi ikagawanywa kwenye madaraja mawili; wageni wakaingia daraja la pili na wenyeji wakawa daraja la kwanza.

Kwa miaka 100 iliyofuata, hapakuwa na ubishi kwamba Ligi Daraja la Kwanza ndiyo ilishika hatamu za soka ya kulipwa nchini England.

Kwa mafanikio yaliyopatikana na maono ya kupata utajiri kutokana na hadhi waliyokwishajijengea, ndipo walianzisha Ligi Kuu inayoendelea hadi sasa.

Ligi iliyoshika nafasi ya kwanza sasa ilifumuliwa nakuwekwa katika mfumo mpya, ikawa na madaraja kuanzia la pili, tatu na la nne. Ligi Daraja la Kwanza imekuja tena kubadilishwa jina na kujulikana kama Ligi ya Ubingwa wa Soka.

Post a Comment

 
Top