Mshambuliaji kinda
wa Manchester United Marcus Rashford ametajwa katika kikosi cha
wachezaji 23 cha Roy Hodgson kwa ajili ya michuano ya Euro 2016
Itakayofanyika nchini Ufaransa.
Rashford, mwenye miaka 18, alipachika bao katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Australia ulioisha kwa England kushinda 2-1.Mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge naye pia amejumuishwa,lakini viungo Andros Townsend wa Newcastle na Danny Drinkwater Leicester City wameachwa.
England watacheza dhidi ya Ureno katika mchezo wao wa mwisho wa kujipima nguvu siku ya Alhamisi wiki hii.
Kikosi kamili Walinda mlango: Joe Hart (Manchester City), Fraser Forster (Southampton), Tom Heaton (Burnley). Walinzi:Gary Cahill (Chelsea), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham Hotspur), Ryan Bertrand (Southampton), Danny Rose (Tottenham Hotspur), Nathaniel Clyne (Liverpool).
Viungo:Dele Alli (Tottenham Hotspur), Ross Barkley (Everton), Eric Dier (Tottenham Hotspur), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Jack Wilshere (Arsenal). Washambuliaji:Wayne Rooney (Manchester United), Harry Kane (Tottenham Hotspur), Jamie Vardy (Leicester City), Daniel Sturridge (Liverpool), Marcus Rashford (Manchester United).
Post a Comment