Wanachama wanne wa
kundi lenye utata la Trollstation katika mtandao wa Youtube wamefungwa
jela kutokana na wizi wa mabavu na utekaji nyara bandia.
Kundi
hilo lilihusishwa katika wizi wa mabavu wa bandia katika eneo la
kumbukumbu za uchoraji mjini London pamoja na utekaji nyara bandia
katika eneo la Tate nchini Uingereza mnamo mwezi Julai 2015.
Idhaa hiyo ilio na wateja 718,000 imejijengea sifa kwa kutengeza video bandia mjini humo.
Mwanachama wa tano alifungwa mnamo mwezi Machi kufuatia utapeli wa tukio la bomu.
''Utapeli
huo huenda waliouona kama wa kawaida,bila kujua kwamba ulikuwa unawapa
dhiki raia wa kawaida ambao wanafaa kuendelea na bishara zao bila
kuogofywa''.
''Tunatumai kwamba kifungo hicho kitakuwa mfano kwa
wale wanaotekeleza vitendo vya utapeli kama hivi ambavyo haviwezi
kukubalika kuendelea mjini London'',alisema Robert Short,afisa wa
mashtaka katika huduma ya Crown Prosecution Service.
Post a Comment