Mgombea urais wa
chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amesema meya mpya wa
jiji la London ambaye ni Mwislamu hangezuiwa kuzuru Marekani iwapo
pendekezo lake kwamba Waislamu wazuiwe kwa muda kuingia Marekani
lingetekelezwa.
Kwa sababu ya imani yake, meya huyo mpya Sadiq
Khan amesema ana shaka kuhusu iwapo ataruhusiwa kuzuru Marekani iwapo Bw
Trump atachaguliwa kuwa rais.Bw Trump alipendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani baada ya watu 130 kuuawa kwenye mashambulio ya kigaidi mjini Paris Novemba mwaka jana na baadaye shambulio la San Bernardino, California lililoua watu 14.
“Kutakuwa na hali za kipekee,” mfanyabisahara huyo tajiri kutoka New York amesema.
Pendekezo la Bw Trump lilishutumiwa sana Marekani nan je ya nchi hiyo lakini mwanasiasa huyo amezidi kutetea pendekezo hilo akisema hatua hiyo inahitajika kuhakikisha usalama wa Marekani.
Bw Trump amesema ana furaha kwamba Bw Khan ataongoza jiji la London.
- Jiji la London lamchagua Meya Muislamu
- Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislamu
- Waislamu wamtaka Trump kuomba Msamaha
Bw Khan, wa chama cha Labour, ambaye ni mwana wa wahamiaji kutoka Pakistan, ndiye meya wa kwanza wa London kuwa Mwislamu.
"Ningependa kwenda Marekani na kukutana na mameya wa miji ya Marekani,” Bw Khan aliambia gazeti la Time.
"Iwapo Donald Trump atachaguliwa kuwa rais, nitazuiwa kufanya hivyo kwa sababu ya imani yangu.”
Aliongeza kwamba ana imani kwamba mtazamo wa Donald Trump kuhusu siasa hautafanikiwa nchini Marekani.
Post a Comment