Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi wa sukari tani 6757 mali ya El-Naeem Enterprises iliyokamatwa hivi karibuni katika bohari ya forodha ambapo imesema kuwa ilikuwa chini ya uangalizi ikisubiri vibali husika ili iweze kuruhusiwa kusambazwa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipakodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania, Richard Kayombo, amesema sukari hiyo ilikuwa katika bohari ya forodha ya uangalizi ya mamlaka ya mapato Tanzania ikiwa imehifadhiwa kusubiri kukamilishwa kwa utaratibu wa kodi, vibali vya mamlaka ya chakula na dawa TFDA na vibali vya bodi ya sukari na hatimaye kuweza kuruhusiwa kutoka.
CUE IN: RICHARD KAYOMBO, Mkurugenzi wa elimu kwa mlipa kodi TRA
Sukari hiyo kwa sasa imeruhusiwa kutolewa ambapo Channel Ten imefika katika bohari hiyo ya forodha na kushuhudia ikipakuliwa tayari kusambazwa nchini.

Post a Comment