Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya
Mbeya,Nyerembe Munasa Sabi akiongozana na askari wa Jeshi la Polisi
ameingia mitaani kutekeleza agizo la Rais Dk.John Pombe Magufuli la
kuwasaka wafanyabiashara wanaoficha sukari, na ndipo akafanikiwa kubaini
kiwanda bubu cha kufungasha sukari kinachodaiwa kufanya kazi hiyo
kinyume cha sheria na ndipo akaingiwa na hofu kuwa huwenda kiwanda hicho
kinafungasha sukari iliyokwisha muda wake na kuwauzia wananchi.
Baada ya kukamatwa,mmiliki wa kiwanda hicho ambaye pia ni
mfanyabiashara maarufu wa sukari jijini Mbeya,Bushir Sanga yakaibuka
malumbano makali dhidi yake na Mkuu wa wilaya kuhusu aina na uhalali wa
mifuko inamofungashiwa sukari hiyo.
Baada ya kujiridhisha kuwa mfanyabiashara huyo hana kibali cha
kufungasha bidhaa hiyo kutoka kwenye viwanda vya sukari vya ndani ya
nchi,Mkuu huyo wa Wilaya akaamuru mfanyabishara huyo akamatwe ili akatoe
maelezo polisi.
Post a Comment