Rais Obama anayehudhuria mkutano huo anatarajiwa kufanya ziara ya
kihistoria ya kuwa rais wa kwanza wa Marekani kuzuru eneo la Hiroshima
ambalo Marekani ilifanya shambulizi la kwanza kwa bomu la atomiki nchini
Japan.
Mkutano wa viongozi wa mataifa saba tajiri kiviwanda umeanza Alhamisi
katika mji wa Ise Shima nchini Japan. Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe
amewahimiza viongozi wa mataifa hayo kutafuta suluhisho bora kukabiliana
na hali ya uchumi wa dunia unozidi kufifia. Suala kuu linalotarajiwa
kupewa kipaumbele kwenye mkutano huo ni hali ya uchumi duniani pamoja na
ushirikiano katika vita dhidi ya ugaidi.
Kabla ya mkutano huo kuanza waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe alisema
"Kauli mbiu kuu katika mkutano ni jinsi mataifa ya G7 yataitikia hali ya
sasa ya uchumi duniani. Huu ndio wakati wa mataifa ya G7 kushughulikia
hali mbalimbali na ninayo matumaini mkutano utapitisha ujumbe thabiti na
bayana unaojumuisha kuimarisha uchumi thabiti wa ulimwengu"
Hata hivyo huenda muafaka ukakabiliwa na ugumu ikizingatiwa Kansela wa
Ujerumani Angela Merkel alishakataa wazo hilo, wawili hao walipokutana
mapema mwezi huu. Shinzo Abe anasema
Rais wa Marekani Barrack Obama anayehudhuria mkutano huo anatarajiwa
kufanya ziara ya kihistoria ya kuwa rais wa kwanza wa Marekani kuzuru
eneo la Hiroshima ambalo Marekani ilifanya shambulizi la kwanza la bomu
la atomiki tarehe 6 Agosti mwaka 1945. Inahofiwa kuwa ziara hiyo ya
Obama Hiroshima huenda ikapata umaarufu zaidi na kuumeza mkutano
wenyewe.
Suala jingine linalotarajiwa kupewa kipaumbele ni vita dhidi ya ugaidi
ambapo rais wa Ufaransa Francois Hollande anatarajiwa kuzungumzia
mashambulizi mawili ya kigaidi dhidi ya nchi yake mwaka jana.
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron anahudhuria mkutano huo huku
suala la nchi yake kupiga kura ya maamuzi mwezi ujao kujitenga au
kusalia katika Umoja wa Ulaya likitarajiwa kujipenyeza kwenye mkutano
huo.
Viongozi wengine wanaohudhuria mkutano huo ni kansela wa Ujerumani
Angela Merkel, rais wa Ufaransa Francoise Hollande, kiongozi wa Italia
Matteo Renzi na wa Canada Justin Trudeau.
Maafisa wa Japan wamesema wameimarisha usalama huku maelfu ya polisi wakishika doria katika maeneo na vituo mbalimbali.
Post a Comment