0

Mh. Hasan Kaunje
Mbunge wa jimbo La Lindi Mjini Mh. Hasan Kaunje Siku ya Jumamosi ya Tarehe 28/5/2016 aliweza kuzungumza na wapiga kura wake wa jimbo hilo kupitia Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mpilipili.

Kupitia Mkutano huo ameweza kuwashukuru wananchi kwa kuweza kumuamini na kumpa kura ya Ndio katika Uchaguzi wa wabunge na Madiwani uliopita na Kumfanya yeye kuwa mwakilishi katika Bunge la 11.
Mh Kaunje
Aidha Mh Kaunje amesema anafanya kila jitihada kuhakikisha anapambana na Kero mbalimbali zinazolikabili jimbo la Lindi Mjini hasa katika eneo la Upatikanaji wa Maji ya Uhakika.

Kaunje amewahakikishia kuwa yeye ni mbunge imara na yupo bungeni kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi wa Lindi.
Mama Salma Kikwete
Mkutano huoa ulihudhuriwa na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete ambaye alikuwa Mgeni Rasmi.

Post a Comment

 
Top