Kampuni ya mawasiliano nchini TTCL imezindua nembo yake mpya pamoja na Huduma ya 4GLTE ambayo imekuja kuleta ushindani kwenye teknolojia ya mawasiliano.
Uzinduzi huo ambao uliuzuliwa na Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, aliwataka kampuni hiyo ya TTCL kuwa wabunifu kwenye soko la mawasiliano ili kupata faida katika kampuni hiyo.
“TTCL lazima mubadilike ili muweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia na hivyo kumudu ushindani uliopo sasa katika sekta ya mawasiliano”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa pia alizungumza kuwa serikali imetenga masafa ya 800 MHZ ambayo yataiweza kampuni ya TTCL kushindana na makampuni mengine ya watoa huduma mawasiliano na data.
“Uzinduzi wa nembo mpya ya TTCL na huduma ya masafa ya 4G LTE uendane na ubunifu kwa wafanyakazi ili muwavutie watumiaji wengi wa simu na hivyo kupata soko kubwa na kuifanya TTCL kuchangia kikamilifu pato la taifa”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Bi. Edwina Lupembe
amesisitiza kwamba TTCL imejipanga kuboresha huduma za fedha ili
kuwezesha watumiaji wengi wa kampuni hiyo kunufaika na huduma ya kutuma
na kupokea fedha.
“Tumekamilisha
mradi mkubwa wa kusimika mitambo ya GSM, UMTS na LTE ambayo itakuwa na
uwezo wa kutoa huduma ya mawasiliano 2G, 3G na 4G”, amesema Bi. Lupembe
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt.
Kamugisha Kazaura amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa mabadiliko ya
muonekano wa TTCL yataendana na mtazamo mpya wa wafanyakazi wenye lengo
la kuiwezesha kampuni hiyo kuwa ya kisasa hapa nchini.
Amesema
TTCL imejipanga kuboresha simu za mezani, mkononi, na huduma za
intaneti ya haraka ili iweze kupata wateja wengi na hivyo kuongeza
mapato yake.
“Teknolojia
ya 2G GSM, 3G UMTS na LTE imeongeza nguvu kwa kampuni yetu kuleta
ushindani katika soko la mawasiliano na zitaendelea kuongeza ufanisi na
ubunifu wa huduma zetu kwa bei nafuu”, amesisitiza Dkt. Kazaura.
Tayari huduma ya 4G LTE inapatikana katika maeneo mengi ya Ilala, Temeke na Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Post a Comment