Beki wa Toto African, Salum Chuku (katikati) akichuana na mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu (wa pili kushoto) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara
“Kufanya mazoezi katika mazingira magumu bila kujua nitakula nini ni kati ya changamoto kubwa nilizokutana nazo. Katika msimu wangu wa kwanza kucheza ligi kuu, nimejifunza uvumilivu, kwa maana mzunguko wa ligi ni mrefu halafu kuna baadhi ya mechi zinakuwa karibu karibu sana, inabidi ucheze mechi katika kituo kimoja. “
“Bila kupumzika usiku mnapaswa kuanza safari kuwahi mechi nyingine katika kituo kingine ili kuwahi ratiba. Mwanzoni nilikuwa nashindwa ila sasa najiona naanza kuzoea”, anasema mlinzi wa kushoto wa Toto Africans ya Mwanza, Salum Chuku, 21, wakati nilipofanya naye mahojiano marefu hivi karibuni.
Kijana huyo mzaliwa wa Geita alianza maisha yake katika soka la ushindani akiwa nyumbani kwao Geita mwaka 2012 aliposajiliwa timu ya Geita Gold Sports. Aliisaidia timu hiyo kushinda ubingwa wa ‘mabingwa wa mikoa’ mwaka 2013.
“Baada ya kuisaidia Geita kushinda ubingwa niliondoka na kujiunga na Simba B (Timu ya pili ya Simba SC.) Geita wakaenda kucheza ligi ya kanda wakaja kuzungumza na Simba ili nirejee kucheza ligi ya kanda pale Shinyanga mwaka 2014. Wakakubaliana nami nikarejea, Mungu akatusaidia timu ikafanikiwa kupanda hadi ligi daraja la kwanza”, anasema Chuku.
“Baada ya timu kupanda, mimi nikarudi tena Simba B nilikaa kwa muda mrefu kidogo na niliichezea katika mashindano ya vijana ya Rollingstone. Baada ya hapo mwenyekiti wa Chama cha mpira Geita akanifuata na kuuomba uongozi wa Simba B uliokuwa ukiongozwa na Patrick Rweyemamu ili nikaichezee Geita katika ligi daraja la kwanza, hatukupanda. Nikawa na tamani kucheza ligi kuu.”
Anasema Chuku ambaye tayari amecheza game 22 kati ya 28 za timu yake ya Toto Africans msimu huu na kufunga goli moja dhidi ya JKT Mgambo, pia amesaidia kupatikana kwa magoli mengine matatu (assists 3.)
“Timu yangu ya kwanza kwenda baada ya Geita kushindwa kupanda ilikuwa ni Toto Africans. Walikuwa wanajaribu wachezaji nikaenda. Mungu alisaidia nikafanikiwa wakanisajili, ndiyo mpaka sasa niko hapa. Naweza kusema nimepata taabu kwenye mpira kutokana na kwetu nilipotoka hakujulikani ila namshukuru sana Mungu mpaka sasa nipo hapa”, anasema kijana huyo anayemaliza muda wake klabuni Toto mara baada ya kumalizika kwa msimu huu.
“Nitakuwa mchezaji huru baada ya msimu kuisha. Bado sijapata ofa mahala na kama hatotokea nitabaki hapa kwa kuwa nahitaji sana ili kupata uzoefu. Nina ndoto za kurudi tena Simba siku za mbele na kuisaidia
Post a Comment