Watu wa Jamii ya Wawindaji, warina asali, na waokota matunda pori
kutoka kabila la Wahadzabe wanaoishi katika bonde la Yaeda chini wilaya
ya Mbulu wanakabiliwa na tatizo la njaa kali inayodaiwa kusababisha
baadhi ya wanaume kuzikimbia familia zao na kuiomba erikali na taasisi
binafsi zenye uwezo wa kusaidia kupatikana kwa chakula ziwasaidie
kupunguza adha hiyo.Wakizungumza na Ripota wetu wazee wa jamii hiyo
katika kijiji cha Mongoamono wamesema hali imekuwa mbaya kwa upande wao
na watoto ambao ndiyo waathirika wakuu na inadaiwa imesababishwa na
mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa na uharibifu wa mazingira
unaofanywa na watu kutoka jamii nyingi na kwamba hawana njia mbadala ya
kupata chakula.
Kwa upande wao baadhi ya vijana wamesema hivi sasa wanalazimika
kuchimba mizizi hata isiyoliwa ili kuokoa uhai wao,watoto na wazazi wao
kwani hakuna matunda wala wanyamapori kama walivyozoea
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mongoamono Kata ya Yaeda chini Bw. Pascal
Kajema amesema uongozi umeanza kutoa elimu kwa jamii hiyo ili kubadili
mfumo wa maisha yao waweze kujihusisha na shughuli zingine zikiwemo za
kilimo ili kukabiliana na tatizo njaa.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.