0

UPORAJI WA PIKIPIKI WATIKISA LINDI

NA Fadhila Mwanja,Lindi
Uporaji wa pikipiki umeitikisa  mkoani Lindi  kutokana na matukio  ya kikatili   34  yametokea  ndani ya  miezi  mitatau  tangu januari  hadi  machi  mwaka  huu.
 
Hayo yamebainishwa  na  mkuu wa upelelezi  wa jeshi la polisi  nchini DCI  Diwani Athuman wakati alipokuwa anazungumz a  na waandishi wa habari kwenye ziara yake ya kikazi  mkoani hapa.
 
 Athumani amesema kuwa matukio ya uporaji  wa pikipiki  mkoani  humu  yamekuwa  tishio  kwa maisha ya waendesha pikipiki  na abiria  kwani  yameongezeka kutoka 11  mwaka 2015 hadi 34 marchi 2016.
 
 Alisema serikali haiwezi kuwavumilia waalifu  hao  wakiendelea kufanya matendo ya unyanyanyi  na ukatili dhidi ya binadamu  mwengine ambao wanaangaika  kutafuta riziki zao kwa njia halali. 
 
Athumani alisema pia  idara yake haitawavumilia askali polisi idara ya upelelezi wenye tabia  ya uomba na kupokea rushwa kwa lengo la  kuchelewesha na kupotosha ukweli katika kesi kwa visingizo mbalimbali.
 
Aidha alisema seriklai ya awamu tano imejipanga  na imejidhatiti kwenye ukusanyaji wa kodi hivyo  jeshi la polisi lita hakikisha bandari bubu zote zinadhibitiwa ili kupunguza mianya  ya ukwepaji kodi unaofanya na wafanyabiashara wasio wadilifu,Ndugu zangu suala la kodi ni uti  wa mgongo wa taifa lolote duniani kw nafsi hii nawaomba wale wote wanaotumia babdari bubu  kukwepa  kodi  kuacha mara  moja  kabla mkono wa sheria hawajakutanao alisema Athumani

 Kamishna wa makosa ya jinai kwa jeshi la Polisi wa Taifa, Diwani Athumani akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Lindi Jana.

Post a Comment

 
Top