Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi
Aliyekuwa rais wa
shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter ameelezea vile maafisa wa
serikali ya Uswizi walivyomtaka kumsihi rais wa Burundi anayependa soka
Pierre Nkurunziza kujiuzulu kufuatia maandamano dhidi ya uongozi wake
mwaka uliopita,kulingana na jarida la soka duniani.
Madai hayo
yameandikwa katika wasifu wa Seppo Blatter kwa jina Mission &
Passion, Fussball ambalo limechapishwa nchini Ujerumani .Mnamo mwezi Mei ,waziri wa kigeni wa Uswizi Yves Rossier alimtaka Sepp Blatter kumpatia Nkurunziza kazi ya ubalozi wa soka kulingana na jarida hilo.
Bwana Rossier alifanya ombi hilo baada ya kuagizwa na Marekani,lakini mpango huo ukafeli kwa sababu alikuwa na maswala mengine yaliokuwa yakimkabili,bwana Blatter alinukuliwa akisema.
Post a Comment