Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven amemwagiza Kamanda wa Polisi mkoa huo,
Jacob Mwaruanda kuwasaka na kuwakamata watumishi hewa 18 waliobainika
katika uhakiki uliofanyika katika halmashauri zote mkoani humo hivi
karibuni.
Pia
ameagiza fedha hizo zilizolipwa kwa watumishi hao hewa na kuiingizia
hasara kubwa Serikali zirudishwe mara moja. Akifafanua alisema katika
uhakiki huo, watumishi hewa tisa walibainika katika wilaya ya Nkasi,
wanane katika Manispaa ya Sumbawanga na mmoja wilaya ya Sumbawanga
wakati Kalambo ikiwa haina mtumishi hewa.
Uhakiki
huo unatokana na maagizo aliyotoa Rais John Magufuli baada ya kuwaapisha
wakuu wa mikoa aliowateua, aliwaambia wakafanye kazi ya kutatua kero za
wananchi na sio kwenda kufanya siasa. Pia Rais Magufuli aliwapa
wakurugenzi wa halmashauri siku 15 wawatoe katika orodha ya malipo ya
mshahara wafanyakazi hewa wote katika halmashauri zote nchini.
Zelothe
alitoa agizo hilo jana katika kikao maalumu cha kufahamiana
kilichojumuisha wazee, viongozi wa dini , watendaji wa umma na wajumbe
wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo kilichofanyika mjini
hapa. Alisisitiza kuwa hajaridhishwa na uhakiki huo, hivyo akaagiza
halmashuri zote kurudia upya uhakiki wa watumishi.
“Siku ile
ile nilipoapishwa kabla sijavuka geti kutoka nje ya Ikulu nilipiga simu
na kuagiza halmashauri zote (Manispaa, Nkasi, Kalambo na Sumbawanga)
kuanza uhakiki mara moja wasinisubiri hadi niripoti mkoani hapa,”
alieleza.
Aliongeza
kuwa aliporudi mkoani humo na kuripoti kazini katika siku yake ya
kwanza ofisini alikabidhiwa kitabu chenye orodha ya watumishi wa umma wa
halmashauri zote akielezwa kuwa hakuna mtumishi hewa katika mkoa wa
Rukwa.
“Sikukubaliana
nao nilikataa, nikaagiza ufanyike uhakiki mara moja ndipo wamepatikana
watumishi hewa 18 na watumishi wengine 137 wapowapo tu wakiwa na taarifa
zinazotia mashaka. Wote wamebainika kwenye hicho kitabu
nilichokabidhiwa kikionesha hakuna mtumishi hewa,” alisisitiza.
Chanzo: Habari Leo
Post a Comment