Leicester City wametanua uongozi wao kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya
Kandanda ya England kwa pengo la pointi saba baada ya kuwabwaga
Southampton bao moja sifuri katika uwanja wa King Power.
Kocha wao Claudio Ranieri amesema kuwa “wanaiendeleza ndoto yao” bila
shaka akimaanisha kulitwaa kombe la Premier League msimu huu. Leicester
ina pointi 69 kukiwa na mechi sita msimu kukamilika, pointi saba mbele
ya nambari mbili Tottenham Hotspur, ambao wallitoka sare ya moja moja na
Liverpool Jumamosi.
Arsenal ilibakia katika nafasi ya nne, ikiwa na pointi 58 baada ya
kuirarua Watford nne bila huku Manchester City ikisalia ya nne na pointi
54 baada ya kuibambua Bournemouth nne bila. Manchester United nayo
inaendelea kuwinda tikiti ya kumaliza katika nne bora wakati iliifunga
Everton moja bila na kusonga hadi pointi 53.
Arsenal, City na United zote zina mchezo mmoja wa ziada lakini ikiwa
Leicester itashinda mechi zake nne kati ya sita zilizosalia, haiwezi
kufikiwa na itakamilisha mojawapo ya hadithi za kushangaza kabisa katika
historia ya 128 ya ligi ya kandanda ya England.
Post a Comment