Wazazi
na walezi wa shule ya msingi wasiona na wanaona Nyangao wilayani Lindi
wameishauri serikali kuifunga shule hiyo kutokana na kukosa huduma muhimu
ikiwemo chakula kwa wanafunzi hao.
Akizungumza
mwenyekiti wa kamati ya shule Saidi Matipa kwenye hafla ya kukabidhi Baskeli
kwa mtoto mlemavu Fatuma Liulwa uliotolewa na chama cha walimu Mkoa wa Lindi
(CWT) kwa ufadhili wa shirika lisilokuwa la kiserikali Human Bridge jana.
Matipa
alisema kutokana na kutokuwepo kwa huduma ya uhakika ya chakula ni bora
serikali inaifunga shule hiyo ili kunusuru maisha ya watoto hao.
Matipa
alisema awali shule hiyo ilikuwa inatengewa bajeti na serikali shilingi milioni
6 kwa mwenzi lakini hivi sasa inapata shs laki 9 kwa mwenzi jambo linasababisha
huduma za chakula kushuka kwa wanafunzi ambapo wanapata mlo mmoja kwa siku.
Alisema
halmashauri ya wilaya imeitelekeza shule hiyo ambayo kwa sasa ina hudumiwa na
mwalimu mkuu Rashidi Mponda ambaye anatumia hela yake ya mshahara kununulia
chakula, mafuta ya kupikia na mboga.
Awali
katibu wa chama cha walimu mkoa wa Lindi Hamisi Rajabu alisema dhamira ya chama
cha walimu ni kutetea na kupigania maslai ya walimu , kutunga na kusimamia sera
itakayo linda hadhi ya walimu wenye ulemavu kwa kutambua wajibu na haki
maumbile na mazingira ya kazi.
Rajabu
alisema kwa kuwa walimu ni walezi na wazazi kitengo hicho usaidia wanafunzi
wenye ulemavu vifaa visaidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu ili kuwawezesha
kujifunza na kushiriki vyema masomo.
Rajabu
alisema chama kupitia idara ya walimu wenye ulemavu uwajibika kutambua walimu
wake na aina ya ulemavu walio nao ili inapowezekana kuwapatia vifaa vya
kuraisisha kazi zao vinawafika walipo.
Post a Comment