Boko Haram wavamia kambi ya jeshi Nigeria na kuua wanajeshi
Wapiganaji wa kundi
la Boko Haram wameishambulia kambi ya jeshi la Nigeria mapema asubuhi
ya leo na kuua idadi kubwa ya wanajeshi huko Borno.
Idadi kamili ya waliouawa haijajulikana.
Mwanajeshi mmoja aliyeko Borno ameielezea BBC
kuwa''wapiganaji wa Boko Haram waliwavizia na kuwashambulia alfajiri na
mapema wakiwa wamelala.''
''Wapiganaji hao walikuwa wamejihami kwa silaha kali na kusababisha maafa makubwa upande wa wanajeshi''
''Tuliwapoteza wenzetu wengi,,,,,wengi sana,, sijui
hata ni wangapi waliojeruhiwa'' alisema mwanajeshi huyo ambaye hakutaka
kutajwa jina lake
Kambi hiyo ndogo iliyoko katika kijiji cha Kareto
ilikuwa na wanajeshi wachache ambao kazi yao ilikuwa ni kulinda ngome
kabla ya kikosi kikubwa zaidi kuwasili.
Hata hivyo mwanajeshi huyo
anasema kuwa idadi ya wapiganaji hao ilikuwa kubwa mno hata wanajeshi
kadhaa walitoroka ilikuokoa maisha yao.
''Walikuwa na silaha nzito nzito na kali kuliko zetu'' afisa huyo aliiambia idhaa ya BBC Hausa.
Mwanajeshi mmoja aliyeko Borno ameielezea BBC
kuwa''wapiganaji wa Boko Haram waliwavizia na kuwashambulia alfajiri na
mapema wakiwa wamelala.''
''Tuliwapoteza wenzetu wengi,,,,,wengi sana,, sijui hata ni wangapi waliojeruhiwa''
''Baadhi yetu walitoroka maji yalipozidi unga''
''Tuligundua idadi ya wavamizi ilikuwa ni kubwa kuliko yetu'' mwanajeshi mwengine aliiambia shirika la habari la AFP.
'Walikuwa na silaha nzito nzito na kali kuliko zetu'' afisa huyo aliiambia idhaa ya BBC Hausa.
Wapiganaji kadhaa waliuawa katika makabiliano hayo yaliyodumu kwa saa kadhaa kulingana na wenyeji wa kijiji hicho.
Hata
hivyo jeshi lilijitahidi na kuikomboa kambi hiyo baada ya mashambulizi
ya angani kuwasili na kuwaokoa wanajeshi walikuwa wamesakamwa ardhini.
Idadi kamili ya waliouawa haijajulikana.
Post a Comment