0

 Mkuu wa wilaya ya Liwale,Ephraim Mmbaya akiwa kwenye ukumbi wa Halmashauri akiongea na viongozi wa madhebu ya dini zote zilizopo hapa wilayani Liwale jana.
 Baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali walioudhulia kwenye kikao hicho kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa Halmashauri ya wilaya
Kamanda wa polis wilaya ya Liwale Raphael Mwandu aliyekuwa upande wa kulia akiwa na viongozi wengine wa dini
Baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya walioudhulia kwenye kikao cha mkuu wa wilaya ya Liwale kilichofanyika jana.

Na Mwandae Mchungulike na Anna Millanzi,Liwale

Mkuu wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi,Ephraim Mmbaga ametoa agizo la uhakiki wa silaha zote zinazomilikiwa na wananchi ndani ya siku 30 ya mwezi  April na ametoa rahi ya kila  Mtanzania na kila Mzalendo kushiriki katika adhima ya kulinda amani na utulivu wa wilaya na Taifa letu kwa ujumla.

Mkuu wa wilaya ya Liwale, Mh.Ephraim Mmbaga amesema hayo jana kwenye kikao na viongozi  wa madhehebu ya dini,mkurugenzi, kamati ya ulinzi na usalama, wakuu wa idara pamoja na  wadau mbalimbali wa maendeleo kwa niaba ya wananchi wa kata 3  za Liwale mjini ambazo ni Likongowele,Liwale mjini na Liwale B .

Silaha  zote zinazomilikiwa zinatakikiwa kuhakikiwa upya kuanzia April 1 hada april 30 kuanzia ngazi ya  kitongoji hadi ngazi ya wilaya ili kujua kila  anayemiliki siraha nay a aina gani ya siraha ili kupata taarifa sahihi ya siraha hizo.Baadhi ya watu wanamiriki silaha kinyume na utaratibu hasa pale mmiliki halali anapofaliki na mwanafamilia kujimilikisha kinyume na utaratibu.

“ikiwa rais ameenda kuhakiki sihaha yake ni vyema kila mwananchi anayemiliki silaha kufanya hivyo kwa kutii sheria bila shurti”alisema Mmbaga

Pia alisema swala la ulinzi, Amani na utulivu  ni jukumu la kila Mtanzania  hivyo viongozi wa Dini waendelee  kuhamasisha waumini wao maswala hayo huku akisema kuwa umiliki holela wa silaha yaweza kuwa ni sababu mojawapo ya ukosefu wa Amani katika jamii hivyo amewataka viongozi wa Dini kufikisha ujumbe kwa waumini wao kwa kusema kuwa yeyote mwenye siraha ifikapo  april 1 hadi april 30 mmiriki yeyote ahakikishe siraha yake anayomiliki iwe imehakikiwa ili kupata taaarifa sahihi na idadi sahihi ya siraha zinazomilikiwa  kwa uhalali na baini siraha zinazomilikiwa kimakosa.

Mkuu wa wilaya aliwataka viongozi wa dini waendelee kuwahamasishaji  waumini wao takika utekelezaji wa  usafi hivyo amewataka viongozi haokuendelea  kuwahamasisha  waumini kufanya usafi katika makanisa/ misikiti na hata katika majumba yao huku akiwataka Maafisa wanaohusika na mipango miji kuhakikisha majengo ya wafanyabiashara kuwa katika mpangilio mzuri ili wilaya ya Liwale ivutie.

Na amemwagiza  Afisa ardhi kuhakikisha viwanja walivyopewa wananchi maeneo ya mjini visibaki kuwa vichaka badala yake viwanja hiyo vijengwe na visivyofanyiwa kazi vitolewe kwa watu wengine wanaoweza kuviendeleza kwa kujenga  majengo  na majengo ambayo bado hayajaisha ameomba yamaliziwe ili kuzuia vitendo viovu kama ubakaji, upokaji na ngono zembe huku akisisitiza kuwa maeneo yaliyotengwa katika uwanja wa mpira kwa ajili ya biashara yagawiwe kwa  wafanyabiashara ili wapate maeneo ya biashara na kupafanya mji uwe safi wa kuvutia.

Pia alizungumzia  tatizo la chakula katika wilayani Liwale na huku akitaja sababu kuwa hali ya mvua kuwa nyingi zilizonyesha kwa baadhi ya maeneo zimechangia kukosekana kwa chakula lakini kuna changamoto kubwa kuwa  wakulima wanalima wengi mamejikita sana katika mazao ya biashara kuliko ya chakula pia alibainisha kuna changamoto kwa baadhi ya maeneo kuingiliwa na wadudu waharibifu wa mazao kama vile Konokono, viuwavijeshi katika baadhi ya  vijiji  vya Nangano, Kiangara, Kibutuka huku akijaja changamoto nyingine ni kuwa Kilimo kimekuwa ni cha wazee na akina mama vijana hawajishughulishi kwa asilimia kubwa.

Amevipongeza baadhi ya vijiji  kwa kulima sana mazao yanayostahimili ukame kwa kulima viazi katika  vijiji  vya Makata, Mlembwe, Mpigamiti na kusema kuwa kuna haja ya kuweka miundombinu mizuri ya barabara ili kuwarahisishishia wakulima kusafirisha mazao yao vizuri.

Amewataka wanaohusika na maswala ya ardhi ifanyike sensa kwa wamiliki wa mashamba wanayomiliki na kwa yale mashamba ambayo hayamilikiwi na wakulima wagawiwe kwa vijana ili waweze kulima kwa mujibu wa wa agizo  la mkuu wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi alilotamka kuanzia April 1 hadi  Mei 30 wamiliki wote mashamba yao yawe safi na kama hayafanyiwi usafi wapewe watu wanaoweza kuyahudumia.

Mkuu wa wilaya ameshauri wakulima kulima maeneo ya pamoja ili kuepuka wanyama waharibifu kushambulia mazao ilibainisha sababu inayopelekea wanyama kuingia kwenye mashambana na kuharibu mazao au mazao mashamba mengi hayapo sehemu moja,mashamba mengi yako sehemu mbalimbali na mkulima kuhamia sehemu mbali kwa kufuata msitu na kufungua shamba jipya akiwa peke yake ambako ndio makazi ya wanyama wakali , kama wakulima watalima maeneo kwa pamoja wanauwezekano wa  wanyama waharibifu wa mazao kuhama na kuhamia mbali zaidi.

Pia amewaonya watumishi kufanya kazi kwa mazoea,kutoa lugha zisizofaa pale mtu anapohitaji huduma amewataka watumishi kutoa huduma kwa kwa wakati na kwa haki bila kubagaua na amewata wananchi pale mtumishi yeyote anafanya kazi kinyume cha sheria watoe taarifa ili mtumishi huo awezechukuliwa hatua za kisheria  sawa na watumishi wengine yeyote na kuacha tabia  ya baaddhi watu linapotokea tatizo hawalifikishi sehemu husika na kungoja mpaka kiongozi aje ndipo aliseme.

Mkuu wa wilaya amewataka watu binafsi kuwekeza katika sekta ya  Afya na Elimu katika wilaya ya Liwale huku akimpongeza mmiliki wa zahanati ya Agape na Bwana Mussa Mkoyage kwa kuweza kuweza katika sekta ya Afya pia amewapongeza   wawekezaji wa sekta ya Elimu kwani sasa kuna shule  mbili za English Mediaum.

Na amewakumbusha wananchi kwa sasa malipo yanafanyika kwa njia ya Electroniki na amewataka wananchi wanaponunua bidhaa kudai risiti ya bidhaa anayoinunua kwani kupewa risiti ni haki ya kila mteja anaponunua bidhaa kwa kufanya hivyo atakuwa ameisaidia serikali kukusanya kodi na kuweza kuweza kuendesha shughuli zake na kutoa huduma wa wananchi.

Post a Comment

 
Top