
Ligi ya mkoa kituo c:Liwale
Leo kulikuwa na mchezo kati ya Vijana stars Vs Stand warriors mchezo uliochezwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale Mkoani Lindi na matokeo ya leo katika mchezo huu mpaka dakika 90 zinamalizika yalikuwa Vijana stars 1-2 Stand worriors
Magoli ya stand worriors yalifungwa katika dakika ya 3 kupitia kwa mchezaji Msafiri Kambwili na goli la pili lilifungwa na kesi maulidi namo dakik ya 54 na Goli la vijana stars lilifungwa katika dakika ya 37 kupitia mchezaji Faraji Hasani
Kocha wa Stand worriors Ibrahim Hamisi alisema mchezo wa leo ulikuwa mzuri yaliotea ambayo ni mapungufu ni ya kibinadamu japo walipewa kadi nyekundu .
"Nawashukuru wanaliwale kwa kutupokea na kutuona sisi kama wa kwao na sisi tumejisikia kama wa kwao ndio maana tumeweza kujitahidi na kuongoza bidii na ndio timu pekee ya kutokea Lindi mjini" alisema Ibrahim
Kocha wa timu ya Vijana stars alikataa kuongea chochote na nilimtafuta nahodha pia hakuonekana uwanjani.

Kesho kutakuwa na mchezo wa mwisho
Mikukuyumbu world soccer Vs Kijiwe fc
Mpambano unaotarajia kuwa mkali sana
Mikukuyumbu world soccer Vs Kijiwe fc
Mpambano unaotarajia kuwa mkali sana
Post a Comment