Akizungumza katika kikao cha maendeleo ya kata ya Kianyari, mratibu
wa elimu kata hiyo Bw George Bigori, amesema wastani ya watoto mia moja
hadi mia tatu wameandikishwa kuanza darasa la kwanza kwa kila shule
ya msingi katika kata kianyari, idadi ambayo amesema imekuwa kubwa
ukilinganisha na vyumba vya madarasa vilivyopo.
Hata hivyo mratibu huyo wa elimu katika kata hiyo ya Kianyari,
amesema kuwa pamoja na wazazi kutakiwa kuchukua hatua zinazolenga
kupunguza baadhi ya changamoto katika shule hizo, lakini pia halmashauri
ya wilaya ya Butiama kupitia idara ya elimu imetangaza kuchukua hatua
kali kwa walimu wakuu ikiwa ni pamoja na kuwavua nyadhifa zao endapo
itabaini kuna mwanafunzi amefika darasa la tatu bila kujua kusoma,
kuandika na kuhesabu.
Post a Comment